Swali zuri sana hili. Unaweza kulijibu?
Yesu Kristo hakukamatwa, hakuhukumiwa wala kuuawa msalabani, kwa sababu alishindwa kuyazuia hayo yote yasitokee, bali aliyaruhusu na kuyakubali yote hayo ili kuwafundisha wanadamu juu ya upendo wa Mungu. Alikuwa anatimiza kauli zake za awali:
"Hakuna upendo unaozidi huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwaajili ya rafiki zake". Yesu amewafanya wanadamu kuwa marafiki wa Mungu.
Tena akasema: "Siwaiti tena ninyi watumwa, bali rafiki zangu, mkiyatenda hayo iliyowaamuru"
Roho ya msamaha:
Yesu akiwa msalabani, kabla ya kufa, akasema, "Baba uwasamehe kwa kuwa hawajui watendalo". Yaani anawaombea msamaha wauaji wake.
Na anakuja kudhihirisha baadaye baada ya kufufuka, kuwa alikufa kwa hiari yake:
"Niliutoa uhai wangu kwa hiari ili niupokee tena"
Yesu kwa kuja Duniani, aliyaacha mamlaka yake yote kwa Mungu Baba ili yeye atendewe kama mwanadamu. Baada ya kumaliza majukumu yake, akiwa amejifanya mwanadamu, anaporudia tena utukufu wake aliokuwa nao kabla, anasema:
"Baba unirudishie ule utukufu niiokuwa nao pamoja nawe, kabla Ulimwengu haujakuwako".
Kama Mungu anaweza kuzifanya nyota, mwezi, jua, viwe angani, kinamshinda nini sehemu ya nafsi yake kupaa au hata kutembea angani pasipo na pa kukanyaga wala kujishikilia?