Hivi yule "Baba wa Demokrasia" wa kuigwa na TZ kutoka nchi jirani ni NANI TENA?

Hivi yule "Baba wa Demokrasia" wa kuigwa na TZ kutoka nchi jirani ni NANI TENA?

Kifyatu

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2010
Posts
3,382
Reaction score
3,220
Wale walionengua na kuishinikiza TZ iige mfano mzuri wa "Baba wa Demokrasia" wa Afrika kutoka nchi jirani waje hapa wajieleze.

Nyie mlipaswa kuhudhuria kongamano la [HASHTAG]#MezaYaWazalendo[/HASHTAG] lililofanywa jana ili mjifunze maana ya UZALENDO.

Nyie kila kukicha mnadharau vyenu na kusifia vya wenzenu. Sasa msifieni tena huyu baba yenu wa demokrasia anaewatusi majaji walioamua uchaguzi urudiwe.
 
We niite vyovyote tu. Nimechoka na hii tabia ya upinzani kila siku kusifia mambo ya nje na kuwasaidia wezi wa nje dhidi ya nchi yao. Mmeumbuka leo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni wanachama wa chama gani walisaini mikataba ya wizi ? nani anavunja mikataba na kuifanya nchi ilipe fedha nyingi? Jibu hayo maswali, utajitafakari upya maandishi yako!
 
Ni wanachama wa chama gani walisaini mikataba ya wizi ? nani anavunja mikataba na kuifanya nchi ilipe fedha nyingi? Jibu hayo maswali, utajitafakari upya maandishi yako!
Wa chadema ( sumaye, lowasa) maana wao walishawahi kuwa mawaziri mkuu..mkataba wa buzwagi ulisainiwa uingereza na karamagi lowasa akishuhudia..kwa maelezo zaidi muulize saed kubenea wa mwanahalisi
 
Wa chadema ( sumaye, lowasa) maana wao walishawahi kuwa mawaziri mkuu..mkataba wa buzwagi ulisainiwa uingereza na karamagi lowasa akishuhudia..kwa maelezo zaidi muulize saed kubenea wa mwanahalisi
ILANI YA CCM NDIYO ILIYOTUMIKA, SIYO YA LOWASA WALA SUMAYE. MUONGOZO UNATOLEWA NA CHAMA UNAENDA KWA WATENDAJI WAKE.
 
Alianza vizuri juzi, jana akateleza mihemko ya kwenye jukwaa! lakini bado huwezi linganisha na nchi yoyote ya kiafrika. Hopefully atarekebisha alipoteleza.
Ameahidi kuwa uchaguzi huu ukiisha atawashughulikia kweli kweli (na watakiona cha mtema kuni) wale majaji "wakora". Yaliyoko kwenye mibano ni nyongeza yangu nikimuenzi Lissu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii post braza umegonga watu kwenye nyonga..wao wanadhani demokrasia rahisi kiivyo wakati wenyewe kwenye chama tu imewashinda..halafu wanataka wenzao wa practice ili iwe njia nyepesi kwao..tutangoja kwanza iingie kwenye chama chao kisha tutaiga wanavyoitendea haki hiyo demokrasia..
 
Basi watu wote walioko upinzani ni MALAIKA wa NURU, Na INNOCENT wakombozi wanapigania wanyonge kuliko hata maisha yao binafsi na hawajawahi kulikosea TAIFA HILI
WAMETOKA KWENYE KUNDI LA SHETANI SASA WAKO KUNDI LA MALAIKA, WAKIRUDI TU HUKO WANAKUWA MASHETANI TENA. ANGALIA UONEVE, UVUNJWAJI WA KATIBA, SHERIA, UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU, UONEVU, UKATILI UNAOFANYIKA SASA. BADO NI CHAMA HICHO HICHO....
 
Hii post braza umegonga watu kwenye nyonga..wao wanadhani demokrasia rahisi kiivyo wakati wenyewe kwenye chama tu imewashinda..halafu wanataka wenzao wa practice ili iwe njia nyepesi kwao..tutangoja kwanza iingie kwenye chama chao kisha tutaiga wanavyoitendea haki hiyo demokrasia..
Hakuna alichogonga, bado Kenya wamejitahidi. Huwezi kumkamata mpinzani kwa uonevu kama ilivyo hapa, katiba haivunjwi hovyo hovyo kama hapa, haki za binadamu hazivunjwi wazi wazi kama hapa. Bado pamoja na mapungufu yao, wako mbele afrika nzima. Tumeoza wote, lakini kunuka tunatofautiana.
 
Ni wanachama wa chama gani walisaini mikataba ya wizi ? nani anavunja mikataba na kuifanya nchi ilipe fedha nyingi? Jibu hayo maswali, utajitafakari upya maandishi yako!
Vitu vingine usikurupuke kama umeishiwa hoja, huyu anazungumzia demokrasia, wewe unakuja na kusaini mikataba ya wizi, jenga hoja dhidi ya aliyoitoa then uanzishe mada juu ya mikataba.
Tunaboa tunapokuwa tunakurukia rukia mambo, jibu hoja husika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna alichogonga, bado Kenya wamejitahidi. Huwezi kumkamata mpinzani kwa uonevu kama ilivyo hapa, katiba haivunjwi hovyo hovyo kama hapa, haki za binadamu hazivunjwi wazi wazi kama hapa. Bado pamoja na mapungufu yao, wako mbele afrika nzima. Tumeoza wote, lakini kunuka tunatofautiana.
Lakini ni ruksa
- kumuua mkuu wa TEHAMA wa tume ya uchaguzi,
- kuchukua nywila (vidole na kiganja) zake,
- kudukua mtandao wa matokeo ya uchaguzi,
- halafu mkatae seva zenu zikaguliwe na mahakama.

Yote haya kwa jina la demokrasia, eh?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom