Tanzania ina mapungufu mengi kiutawala. At least Magufuli anajaribu kurekebisha uozo uliokuwepo hapo nyuma. Lakini ninachokisikia kutoka upinzani ni kumkalia kooni tu kwa kila jema analofanya.
Nchi hii ilikuwa imepamba kasi kuelekea kusiko. Tumepata rubani alieamua "kutobadilisha gia angani" bali kupiga kona ya nguvu kuelekea tunapopaswa kwenda.
Sasa katika huu mbadiliko wa ghafla wa mwelekeo abiria lazima wayumbe ndani ya chombo. Hili ni la mpito tu.
Tukishazoea muelekeo mpya tutatulia na wengi wataelewa kwa nini tunapitia huu msukosuko.
Hakikisha tu kuwa umefunga mkanda.
Sent using
Jamii Forums mobile app