Hivi yupo wapi msanii Tekno wa kipindi cha nyuma

Hivi yupo wapi msanii Tekno wa kipindi cha nyuma

Huo mkwaju unamwezi tangia autoee alikuwa anaumwa koo kama ommy dimpoz tuu .. sasa amerudi kwenye game ..
Screenshot_20191209-063231_YouTube.jpeg
 
Huyo tekno ni wa nchi gani mkuu? Anapiga nyimbo gani?
Siku ya kwanza nasikia ngoma inaitwa Duro kutoka kwa Tekno nikasema hii ni hit haiitaji maelezo.

Hakuishia hapo zilifuata ngoma zilizonamba Afrika na zikavuka boda mastaa kibao wa Mamtoni walijirekodi wakicheza.

Hivi yupo wapi Tekno wa kipindi cha nyuma..
Tekno ya Duro, Wash, Diana, Pana, Where, Go, Jogodo, Yawa N.k

Kwa speed ya kipindi kile cha nyuma kidogo Afrika ilianza kumtabiria makubwa kwamba anakuja kuuvunja ufalme wa Davido na StarBoy Wizkid. Japo inaitaji ulale Studio kuwamaliza hao jamaa.

Kwa sasa Naona Tekno Amerudi nyuma kidogo sisikii hit kama zile za mwanzo. hii ngoma yake mpya na Zlatan ina miezi kama miwili na bado ina Views Million 3 youtube.

Wakati Mkwaju kama Pana umejizolea Youtube Viewa milion 115.

Game Ngumu? Au kalizika? Au kuna Jambo linakuja kutoka kwa Tekno?
 
Kuna wakati tekno nimekuwa obsessed naye kabisa.
Yaani bila kusikia ngoma yake nilikuwa sielewi kabisa mpaka wadau wakaniitaga tekno chuoni.
Tekno aliugua koo, inaweza ikawa ndo sababu amekaa sana bila kuimba tena lakin vile vile ni producer, kaproduce ngoma kali kibao tu.
 
kama unaongelea kiki na kutrend kwenye Media basi jamaa yuko kimya kwa muda, ila kama unaongelea ngoma kali jamaa bado yupo vizuri sana isikilize ngoma yake mpya Skeletum utajua jamaa bado yupo vizuri
 
Tecno me namuelewA Sana tena mno. Alikuwa anaumwa cancer ya koo nadhan saizi yupo vizuri
 
Diana na where, ndio nyimbo nzuri nazozikubali mpaka kesho. Duro beat limetulia sana hasa ukisikilizia kwenye home theatre. If, ikawa nyongeza, sijui jamaa ndio alipiga beat la follow ya davido!!
 
Back
Top Bottom