Lord Diplock MR
JF-Expert Member
- Mar 16, 2015
- 1,446
- 3,319
Nimesikia habari za Maridhiano na nimesikia ujio wa Rais Mstaafu wa nchi jirani kujaribu kukutana na vyama vya siasa nchini na kufanya mazungumzo ya maridhiano. Mazungumzo hayo yanatarajiwa kufanyika kwa muda wa siku kadhaa kuanzia kesho.
Wakati hayo yakiendelea sote tunajua kuwa lipo zuio halali la Mahakama linalowazuia viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kushiriki siasa na kutumia rasilimali za chama. Zuio hilo halali kabisa kisheria lililotolewa na Moja ya Mahakama za juu nchini Tanzania yaani Mahakama kuu kisheria linapaswa kuheshimiwa na wahusika. Kama hiyo haitoshi yapo maombi mbele ya Mahakama hiyo hiyo yakitaka viongozi wakuu wa CHADEMA wakamatwe kwa kukiuka amri hiyo.
Sasa ninachojiuliza ni je zuio hilo linahusu vikao vya maridhiano au hivyo wanaweza kufanya tu kama vile siyo sehemu ya shughuli za kisiasa?