PostGE2025 Hivi, zuio la CHADEMA kushiriki siasa halihusu vikao vya maridhiano?

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Lord Diplock MR

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2015
Posts
1,446
Reaction score
3,319
Nimesikia habari za Maridhiano na nimesikia ujio wa Rais Mstaafu wa nchi jirani kujaribu kukutana na vyama vya siasa nchini na kufanya mazungumzo ya maridhiano. Mazungumzo hayo yanatarajiwa kufanyika kwa muda wa siku kadhaa kuanzia kesho.

Wakati hayo yakiendelea sote tunajua kuwa lipo zuio halali la Mahakama linalowazuia viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kushiriki siasa na kutumia rasilimali za chama. Zuio hilo halali kabisa kisheria lililotolewa na Moja ya Mahakama za juu nchini Tanzania yaani Mahakama kuu kisheria linapaswa kuheshimiwa na wahusika. Kama hiyo haitoshi yapo maombi mbele ya Mahakama hiyo hiyo yakitaka viongozi wakuu wa CHADEMA wakamatwe kwa kukiuka amri hiyo.

Sasa ninachojiuliza ni je zuio hilo linahusu vikao vya maridhiano au hivyo wanaweza kufanya tu kama vile siyo sehemu ya shughuli za kisiasa?
 
UPUMBAVU MTUPU NI KUPOTEZA MUDA ...SULUHISHO LA UKOMBOZI WA TAIFA LETU KWA HAPO TULIPO FIKIA NI NJIA YA DAMU TU..
 
Maridhiano na chauma, act, na chama cha yule jamaa anamuiga Traole na ahadi zake za kiwaki.

Vyama vyote ni matawi ya ccm sijui hayo maridhiano wanafanya na nani.
Kama ni kwasababu ya maandamano, yale maandamano hayakua na kiongozi.
 
UN wamemleta Mchungaji L.Chakwera ndio msimamizi wa maridhiano ya mchongo.
 
Huyo Chakwera awaambie tu kwamba uchaguzi urudiwe na msimamizi huru. Hao commonwealth waje wausimamie ndio mambo yaende. CCM sidhani kama watakubari, Chakwera na commonwealth yake watapoteza muda tu... D9 ndio kilele cha kumuondoka kizimkazi huko magogoni au Mtumba Dodoma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…