Hiyo Dar yenu inapigwa bao siku si nyingi

Hiyo Dar yenu inapigwa bao siku si nyingi

1697778701426.jpg
 
Waziri wa Nishati, January Makamba leo amewasilisha Bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2022/2023 ambapo amesema "Serikali kupitia TPDC imepanga kutekeleza mradi wa ujenzi wa vituo vya kujazia Gesi asilia kwenye Magari katika Bohari Kuu za mafuta za Serikali za Dar es Salaam na Dodoma"

"Lengo ni kuwezesha magari mengi zaidi ya Serikali na watu binafsi kutumia gesi asilia inayozalishwa nchini badala ya Mafuta"

"Serikali kupitia TPDC inayo maeneo kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya uhifadhi mafuta (tank farms) katika maeneo ya kimkakati nchini ili kurahisisha usambazaji wa mafuta kwa nyakati zote, maeneo hayo yapo Kigamboni (Dar es Salaam), Chongoleani (Tanga), Zuzu (Dodoma), Isaka (Shinyanga), Makambako (Njombe), Kibirizi (Kigoma) na Mpanda (Katavi)"
#MillardAyoBUNGENI
 
Wakuu ni hivi kutokana Hali ilivyosasa naona kuna kila sababu ambayo itaitoa dar kama namba moja katika swala Zima la uchumi. Sababu ni hizi.

1. Kuhamishwa Kwa ikulu na ofisi za serikali. Hii imepunguza idadi kubwa ya watu ambao wangelazimika kusafiri na kuwepo mjini Dar. Hivyo imepunguza wananuzi wa mahitaji na huduma mji dar es salaam.

2. Ujenzi wa SGR ya Dar Hadi Dodoma hii itapelekea kuhamishwa kwa viwanda vingi kwani vikiwepo dodoma kutakua na uraisi wa usafirishaji wa mizigo na magarifi kutoka mikoa mingine. Pia viwanda vingi vitapenda kuwa karibu na ofisi za serikali.

3. Ujenzi wa miundo mbinu Bora Kwa mikoa mingine Kwa kipindi kifupi kilichopita tumeshuhudia ujenzi wa miundo yenye tija Kwa mikoa mingine Mfano mpango wa upanuzi wa bandari ya mtwara na ya mbambabay pia ujenzi wa reli ya mbambabay Hadi mtwara. Kwa hiyo baadhi ya mizigo itapungua bandari ya Dar pia baadhi ya viwanda vitajengwa huko mtwara.

4. Ukuaji wa science na technology Kwa Sasa rasilimali nyingi ambazo zilikua hazivuniki lakini Kwa Sasa Kwa mashine za kisasa za bei nafuu. Zimefanya hata wazawa na wageni wakizitumia kuvuna rasilimali zilipo mkoani Mfano iringa kumekuwepo na viwanda vingi vya playwood ambavyo Kwa Sasa vingi vinamatawi njombe hivi vimeifanya Dar kupunyuliwa mkiani Kwa uchumi na iringa na uwepo wa solar na bodaboda n.k umefanya watu waweze kulima hata sehemu za mbali.

5.Ukuwaji wa center nyingine za kibiashara kama vile mwanza, makambako na dodoma kutapunzuza umaarufu wa dar.


Karibu Kwa mjadala
Bandari ya kusafirisha mixigo. Nayo itajengwa Dodoma
 
Back
Top Bottom