Hiyo Dar yenu inapigwa bao siku si nyingi

Waziri wa Nishati, January Makamba leo amewasilisha Bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2022/2023 ambapo amesema "Serikali kupitia TPDC imepanga kutekeleza mradi wa ujenzi wa vituo vya kujazia Gesi asilia kwenye Magari katika Bohari Kuu za mafuta za Serikali za Dar es Salaam na Dodoma"

"Lengo ni kuwezesha magari mengi zaidi ya Serikali na watu binafsi kutumia gesi asilia inayozalishwa nchini badala ya Mafuta"

"Serikali kupitia TPDC inayo maeneo kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya uhifadhi mafuta (tank farms) katika maeneo ya kimkakati nchini ili kurahisisha usambazaji wa mafuta kwa nyakati zote, maeneo hayo yapo Kigamboni (Dar es Salaam), Chongoleani (Tanga), Zuzu (Dodoma), Isaka (Shinyanga), Makambako (Njombe), Kibirizi (Kigoma) na Mpanda (Katavi)"
#MillardAyoBUNGENI
 
Bandari ya kusafirisha mixigo. Nayo itajengwa Dodoma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…