Hiyo Tarehe 29 Hali itakavyokua huko staff

Hiyo Tarehe 29 Hali itakavyokua huko staff

SEHEMU YA PILI

Huo ulikuwa utani hebu tuje kwenye hoja sasa

Soma hoja hizo



HOJA YA KWANZA
Likizo za wanafunzi zipo hivi =
a) Likizo ya mwezi wa nne week mbili=14
b) Likizo ya mwezi wa sita = siku 30
c) Likizo ya mwezi wa tisa siku= 14
d) Likizo ya mwezi wa kumi na mbili = siku 30
Ukijumlisha hizo namba ni miezi mitatu.
Ukiangalia hapo utagundua ni sawa na kusema Likizo za mwaka mzima ambazo zipo kisheria kabisa zimewekwa sehemu moja hivyo mwanafunzi hajapoteza mda wake wowote. Ndiyo hii miezi mitatu ambayo wanafunzi wamekuwa nyumbani kwa ajili ya korona.

HOJA YA PILI 2
Siku ambazo wanafunzi wanapaswa kukaa darasani akifundishwa hazijapunguzwa hata siku moja (194-197) kama hatuamini zihesabu na ndiyo maana tarehe ya kufungwa imesogezwa hadi tarehe 18/12/2020 ili ziweze kukamilika. Hesabu kuanzia shule ilipofunguliwa tarehe 07/01/2020 - 17/03/2020 na tarehe 29/06/2020 - 18/12/2020 utagundua hakuna kupunjwa.

HOJA YA TATU
Pamoja na ukweli kwamba siku za kusoma (194-197) zipo sawa kabisa lakini maelekezo ya serikali ni kwamba yaongezwe masaa mawili kila siku za masomo hivyo mda wa masomo (unaweza ukaanza 07:00 asubuhi-5:30 jioni). Kisheria hapa itabidi shule iingie mfukoni kuwalipa waalimu mda ulioongezwa (over time) fedha ambayo nina hakika haipo kwenye bajeti. Kwa sehemu kubwa hapa walio na faida ni watoto kwa sababu kwenye siku za masomo wameongezewa masaa mawili kila siku za ufundishaji. HUU SI MSAAFU NI MAWAZO TU.
Mwezi wa nane pia kama nilimsikia vizuri waziri alisema kutakuwa na "kijilikizo", nadhani hicho ndo kitakaviwa na hayo masaa mawili.
 
Mimi: sa sikiliza shule ndo hivyo mnafungua tarehe 29 hiyo mimba Fanya kuitoa mapema wasigundue usije kuniletea matatizo nina wazazi wananitegemea


Eliza: hapana mi naogopa kufa halafu pia ni dhambi


mimi : eboo yani mi nikafie jela kisa uwoga wako embu acha mambo yako ya ajabu ndo nshasema hivyo kesho tunaenda toa
 
Mimi: sa sikiliza shule ndo hivyo mnafungua tarehe 29 hiyo mimba Fanya kuitoa mapema wasigundue usije kuniletea matatizo nina wazazi wananitegemea


Eliza: hapana mi naogopa kufa halafu pia ni dhambi


mimi : eboo yani mi nikafie jela kisa uwoga wako embu acha mambo yako ya ajabu ndo nshasema hivyo kesho tunaenda toa
[emoji119][emoji119][emoji87][emoji87][emoji23][emoji23][emoji23]
 
PICHA LINAANZA
"Yule Mwalimu aliyezoea kuwahi kama kawaida saa 12:30 tayari yupo shuleni"

MUDA UNAZIDI KWENDA
Walimu karibu wote wameshafika staff

MARA GHAFLA
"Kanaingia kale ka madam kazuri kuliko wote staff. Kanaonekana kamekonda kidogo tofauti na mwanzo. Kanasalimia"
Miss staff: habari zenu walimu
Wanaitikia walimu wawili tu kati ya walimu 15

WABIASHARA NAO WAPO

Madam Asha: Jamani walimu nauza barakoa
"Walimu wote wanacheka kwa sauti wakuropoka nae karopoka.... Hee hee hee barakoa hizo kwiooo..."

KWA MBALI
Anaonekana mwalim Masamela ndo anaingia shuleni.. walimu wawili wa kike wanamuona kupitia dirisha..
Madam Joy: muoneni yule baba ananikera na suruali lake Lile kama kung'utio la mashineni
Madam Linda: muache baba wa watu kwa raha zake

MTAALUMA NAE
"Jamani walimu kumbukeni kuleta maandalio yenu kabla hamjaingia darasani"
Madam Eliza: we nawe una kihere here Yani watu hata hatujapumua umeanza na maandalio yako...

HUKU MWALIMU MNEMELE NAE ANAMWITA MWANAFUNZI
Mwl MNEMELE: "Hebu ng'ombe mmoja aje hapa nimtume"
MARA MWALIMU MKUU KAINGIA STAFF..
"Jamani walimu sa nne tutakua na kikao kwa hiyo msiondoke"...
Sir adam: chai ipo boss?
Mkuu: chai ipo ila vitafunwa mtajitegemea
Madam Tunu: Yani niache kwenda kunywa chai ya maziwa kwangu ninywe michai ya rangi iyo kazi sifanyi Mimi

SIR MADENGE NAYE ANAONEKANA ANAPEKUA KWENYE MABOX KISHA ANAANZA KULALAMA
"Yani hii staff bwanaa cku tunafunga shule niliacha vifaa vyangu vyote hapa sijui kuku gani kaja kuvihamisha sivioni
Mwl mkuu: "mwl MADENGE vifaa vyako nilivihamishia maana hapo niliona hapako salama sana"...

NAYE CHAPOMBE WA SHULE ANAWAZA KIMOYOMOYO
"Yani ngoja niombe ruhusa tu niseme naenda hospital nikapumzike nyumbani mie akili yangu Leo haipo sawa"

WALIMU
" wanaanza kuingia darasani mmoja mmoja hatimae ofisini wanabaki walimu wawili tu madam Anne na sir Chande
Madam Anne: niliku miss bebe wangu
Sir chande: mi mwenyewe nilikumiss kweli..

NB: Nawatakia maandaliza mema
Naipenda Sana hii fani ya Ualimu kwakweli!! Mkui umeidadavua poa adi imenipa hamasa ya kupiga kazi[emoji120][emoji108]
 
Hapo kwa madamu anne umapatia kabisa, nilisoma shule moja kulikuwa na ticha anaitwa anne alikuwa ni balaa. Kuna kipindi alikuja mwalimu mzungu kutoka USA kuja kufundisha pale, basi anne akawa anajiwekaweka karibu na mzungu hadi yule mzungu akaenda kushtaki kwa mkuu wa shule.😀😀😀😀
Hilo lizungu lilikuwa boya tu
 
Naipenda Sana hii fani ya Ualimu kwakweli!! Mkui umeidadavua poa adi imenipa hamasa ya kupiga kazi[emoji120][emoji108]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji736][emoji736][emoji736]
 
Alieandika huu Uzi afike kituoni haraka iwezekanavyo..
Ukandamizaji
JamiiForums140089583.jpg
 
Mimi kama professional teacher wa English nimejisikia vibaya mnavyojidai mnatujua.

Mtuache na kazi yetu ya ualimu.
 
Back
Top Bottom