Mogan Mogan
JF-Expert Member
- Jul 6, 2015
- 203
- 144
[emoji1787][emoji1787]PICHA LINAANZA
"Yule Mwalimu aliyezoea kuwahi kama kawaida saa 12:30 tayari yupo shuleni"
MUDA UNAZIDI KWENDA
Walimu karibu wote wameshafika staff
MARA GHAFLA
"Kanaingia kale ka madam kazuri kuliko wote staff. Kanaonekana kamekonda kidogo tofauti na mwanzo. Kanasalimia"
Miss staff: habari zenu walimu
Wanaitikia walimu wawili tu kati ya walimu 15
WABIASHARA NAO WAPO
Madam Asha: Jamani walimu nauza barakoa
"Walimu wote wanacheka kwa sauti wakuropoka nae karopoka.... Hee hee hee barakoa hizo kwiooo..."
KWA MBALI
Anaonekana mwalim Masamela ndo anaingia shuleni.. walimu wawili wa kike wanamuona kupitia dirisha..
Madam Joy: muoneni yule baba ananikera na suruali lake Lile kama kung'utio la mashineni
Madam Linda: muache baba wa watu kwa raha zake
MTAALUMA NAE
"Jamani walimu kumbukeni kuleta maandalio yenu kabla hamjaingia darasani"
Madam Eliza: we nawe una kihere here Yani watu hata hatujapumua umeanza na maandalio yako...
HUKU MWALIMU MNEMELE NAE ANAMWITA MWANAFUNZI
Mwl MNEMELE: "Hebu ng'ombe mmoja aje hapa nimtume"
MARA MWALIMU MKUU KAINGIA STAFF..
"Jamani walimu sa nne tutakua na kikao kwa hiyo msiondoke"...
Sir adam: chai ipo boss?
Mkuu: chai ipo ila vitafunwa mtajitegemea
Madam Tunu: Yani niache kwenda kunywa chai ya maziwa kwangu ninywe michai ya rangi iyo kazi sifanyi Mimi
SIR MADENGE NAYE ANAONEKANA ANAPEKUA KWENYE MABOX KISHA ANAANZA KULALAMA
"Yani hii staff bwanaa cku tunafunga shule niliacha vifaa vyangu vyote hapa sijui kuku gani kaja kuvihamisha sivioni
Mwl mkuu: "mwl MADENGE vifaa vyako nilivihamishia maana hapo niliona hapako salama sana"...
NAYE CHAPOMBE WA SHULE ANAWAZA KIMOYOMOYO
"Yani ngoja niombe ruhusa tu niseme naenda hospital nikapumzike nyumbani mie akili yangu Leo haipo sawa"
WALIMU
" wanaanza kuingia darasani mmoja mmoja hatimae ofisini wanabaki walimu wawili tu madam Anne na sir Chande
Madam Anne: niliku miss bebe wangu
Sir chande: mi mwenyewe nilikumiss kweli..
NB: Nawatakia maandaliza mema