Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Mwalimu mkuu : hivi Mr Mlevi mmoja ndo muda gani wa kuripoti shule mpaka kikao tumemaliza we haupo hivi ni shule gani umeona kuna utaratibu wa hovyo kiasi hicho .
Huku pombe zikiwa bado zipo kichwani akiwa anayumba yumba kidogo huku amevaa shati lake limejikunja halijapigwa pasi na suruali nyeusi iliyopauka anajibu
Mr mlevi mmoja :hii shule au kichuguu .tusichoshane hapa
Mwalimu mkuu: halafu unakujaje umelewa hayo sio maadili ya kazi kwanza utafundishaje
Mr mlevi : hizi ng'ombe unadhani zinaelewa basi halafu mbona mi sijalewa na hata nikinywa pombe huo ni mshahara wangu we haukuhusu .we mbona unanunua chipsi funga na hatusemi
Mwalimu mkuu : kausha basi we mtu ni mtu mzima ( akimbembeleza kwa sauti ndogo)
Mara madam Anna anadakia maongezi
Madam Anna : jamani sio vizuri Mr mlevi unachofanya unajishushia heshima hata wanafunzi wanakucheka huoni una jina zuri lakini wanafunzi washakupa nick name mwalimu mlevi
Mr mlevi : hakuna mwalimu ambae hana nick name we mwenyewe wanakuita madam cha wote .eti unajijushia heshima ( huku akiigiza sauti ya madam Anna kwa kebehi ) .kama ungekuwa unaijua heshima usingekuwa unagongwa na kila mwalimu wa field anaye kuja unadhani hatujui
Mr mlevi anatoka ofsini akipiga mluzi akielekea darasa la saba kufundisha hesabu
Akiwa darasani
Wanafunzi : shikamoo mwalimuuuu
Mr mlevi: sitaki salamu zenu na siku nikija kugundua ananiita mlevi nitakuja kumpiga mabanzi *****
Wanafunzi wanacheka
Mr mlevi : halafu Merry nilikwambia unione haukuja hii ni dharau kwahyo mi ni ng'ombe sio
"Kung'utio la mashineni" [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]PICHA LINAANZA
"Yule Mwalimu aliyezoea kuwahi kama kawaida saa 12:30 tayari yupo shuleni"
MUDA UNAZIDI KWENDA
Walimu karibu wote wameshafika staff
MARA GHAFLA
"Kanaingia kale ka madam kazuri kuliko wote staff. Kanaonekana kamekonda kidogo tofauti na mwanzo. Kanasalimia"
Miss staff: habari zenu walimu
Wanaitikia walimu wawili tu kati ya walimu 15
WABIASHARA NAO WAPO
Madam Asha: Jamani walimu nauza barakoa
"Walimu wote wanacheka kwa sauti wakuropoka nae karopoka.... Hee hee hee barakoa hizo kwiooo..."
KWA MBALI
Anaonekana mwalim Masamela ndo anaingia shuleni.. walimu wawili wa kike wanamuona kupitia dirisha..
Madam Joy: muoneni yule baba ananikera na suruali lake Lile kama kung'utio la mashineni
Madam Linda: muache baba wa watu kwa raha zake
MTAALUMA NAE
"Jamani walimu kumbukeni kuleta maandalio yenu kabla hamjaingia darasani"
Madam Eliza: we nawe una kihere here Yani watu hata hatujapumua umeanza na maandalio yako...
HUKU MWALIMU MNEMELE NAE ANAMWITA MWANAFUNZI
Mwl MNEMELE: "Hebu ng'ombe mmoja aje hapa nimtume"
MARA MWALIMU MKUU KAINGIA STAFF..
"Jamani walimu sa nne tutakua na kikao kwa hiyo msiondoke"...
Sir adam: chai ipo boss?
Mkuu: chai ipo ila vitafunwa mtajitegemea
Madam Tunu: Yani niache kwenda kunywa chai ya maziwa kwangu ninywe michai ya rangi iyo kazi sifanyi Mimi
SIR MADENGE NAYE ANAONEKANA ANAPEKUA KWENYE MABOX KISHA ANAANZA KULALAMA
"Yani hii staff bwanaa cku tunafunga shule niliacha vifaa vyangu vyote hapa sijui kuku gani kaja kuvihamisha sivioni
Mwl mkuu: "mwl MADENGE vifaa vyako nilivihamishia maana hapo niliona hapako salama sana"...
NAYE CHAPOMBE WA SHULE ANAWAZA KIMOYOMOYO
"Yani ngoja niombe ruhusa tu niseme naenda hospital nikapumzike nyumbani mie akili yangu Leo haipo sawa"
WALIMU
" wanaanza kuingia darasani mmoja mmoja hatimae ofisini wanabaki walimu wawili tu madam Anne na sir Chande
Madam Anne: niliku miss bebe wangu
Sir chande: mi mwenyewe nilikumiss kweli..
NB: Nawatakia maandaliza mema
Duuh