Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 57,951
- 32,619
- Thread starter
- #21
REACTION TIME
Barabarani nyakati zote hususani inapotokea ajali kuna kitu kinaitwa reaction time, yaani muda unaotumika na dereva au mwili kuitikia kichochea na kuchukua hatua fulani kuepusha hatari iliyopo mbele yake.
Reaction time hutofautiana kati ya dereva na dereva, na hutegemea ukubwa wa hatari, uzoefu, na spidi ya chombo kwa wakati huo.
Jinsi dereva anavyochelewa kureact ndivyo uwezekano wa kutokea ajali au madhara ya ajali kuongezeka huwa mkubwa. Mathalani mtu anapoongea na simu huku akiendesha ghafla kikatokea kitu mbele yake muda atakaotumia kureact utakuwa mrefu kuliko asipokuwa na simu.
Mwingine ikitokea hatari mbele yake badala ya kureact anapigwa butwaa kwanza kwa sekunde kadhaa asijue la kufanya, kisha baada ya hapo akili ndipo zinamrudi kumwambia Kimbia, au toa gari nje ya barabara, nk.
Reaction time(t/r) inahusu pia muda mtu anaotumia kufanya maamuzi hata pasipokuwa na hatari. Mfano, muda anaotumia dereva kuona sasa taa ni kijani naweza kwenda, na hivyo akaamua kuachia brake na kukanyaga eksireta gari iende. Mtu aliyekuwa busy na kitu kingine atareact kwa kuchelewa hadi anapigiwa honi au wenzie wanampita.
Reaction time ni kati ya sekunde 0.7 hadi 3.0. Nchi nyingine duniani huwapima madereva kuona reaction time yao itakuwaje na itachukua muda gani kunapotokea hali tofauti tofauti barabarani.
Tabia yoyote ya dereva inayomfanya dereva kuchelewa kuchukua maamuzi au kuchukua muda mrefu kung'amua jambo na kufanya maamuzi inamuweka dereva huyo katika hatari kubwa ya kupata ajali. Hii inahusisha vitu 3:
-Muda dereva anaopaswa kutambua anapaswa kufanya jambo fulani
-Muda anaotumia kufanya jambo lenyewe
- Muda unaotumika na mfumo wa gari kupokea amri za dereva.
Kwa mujibu wa tafiti, dereva wa wastani anatumia 3/4 ya sekunde kutambua hatari, na 3/4 ya sekunde kutumia breki.
Baadhi ya vitu vinavyoathiri reaction time ni kama vile.
1. Kilevi mwilini
2. Kufuatana kwa karibu (tailgating)
3. Matumizi ya simu
4. Spidi ya kupindukia (excessive speed)
5. Uchovu.
6. Ujuzi hafifu
8. Kukosa uzoefu
Tunashauriwa tupunguze au kuepuka vitu hivi ili kujiepusha na ajali.
RSAadmin1
RSA Tanzania
Usalama Barabarani ni Jukumu Letu Sote.