Hizi alama/maandishi kwenye barabara huwakilisha kitu gani?

Zekoddo

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
1,859
Reaction score
4,539
Naona sana nikisafiri kwenda mikoa tofautitofauti hizi alama/mabango kwenye barabara, mfano; T6 Dar es Salaam au T4 Mtwara.

Huwa zinamaanisha nini wazee wa RoadSite?
 
T1 au Trunk Road 1 ni barabara za Kitaifa mfano
T1 ni Dar es Salaam to Zambia
T2 Chalinze to Namanga (Kenya)
T3 Morogoro to Rwanda
 
Toeni jibu kama mnajua...acheni masihara wengine tunajifunza kupitia hizi forum hapa jf. Jf ni zaidi ya darasa.
Barabara kuu ya kitaifa na kila moja ina namba/ code mf ya dar - tunduma ina namba yake moja,ya dar Arusha,dar mza nk. Code inaanza na T
 
T inamaanisha makutano/junction. Na hizo T1 ,T2 zinaonyesha uelekeo kwenye makutano au baada ya makutano
 
Trunk Road.
T 1 Ni hii ya Dar mpaka Moro.
Chz Sgr in namba yake,
Tan/ Msh nayo Ina code yake.
 
Naona sana nikisafiri kwenda mikoa tofautitofauti hizi alama/mabango kwenye barabara, mfano; T6 Dar es Salaam au T4 Mtwara.

Huwa zinamaanisha nini wazee wa RoadSite?
Bila picha ni umbea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…