Kama hoja ilivyo, naomba wajuvi wa jambo hili la sensa wanieleweshe. Nimeona taarifa zikiandikwa kutoka kwa mamlaka za sensa kuwa hadi sasa kaya zilizohesabiwa ni asimia 93. Ili kupata asilimia lazima uwe na idadi halisi ya jumla ya kaya ambayo ni kamili ndipo ulinganishe na zilizokwisha hesabiwa. La si hivyo hiyo jumla ya kutafutia asilimia iwe ni ya kukadiria.
Nafikiri ingekuwa vizuri wakaandika idadi ya kaya zilizohesabiwa na si asilimia maana sensa yenyewe inatafuta jumla ya idadi ya kaya. Wakiandika asilimia inaleta picha kwamba tayari wanajua kwa ukamilifu idadi ya kaya hata kabla ya sensa hii, ila wakiandika idadi tu ni sawa maana itaendelea kuongezeka.
Naomba ufafanuzi.