Education ndio nimesomea, nikiwa mwaka wa mwisho nimekisoma kitabu cha rich dad poor dad nikaja mbio mtaani Toka mwaka Jana Kuja kufanya biashara lakini inaonekana mfumo wa Sasa kujiajiri Labda kama Huna majukumu utaona pesa inakaa ndani vinginevyo hapo vice versa!
Katika kutafakari na jinsi biashara ilivyo slow nimeona nitafute ajira na niingilie Gia ya kujitolea shule ya secondary iliyopo jirani Nami ili walau nifungue channel nyingine ya pesa (Kwa badae). Target yangu 1kwa1 kwa afisa elimu alie jirani Nami nikamweleze hii Nia yangu!
Mpaka hapo utakua umenielewa msomaji karibu kwa kushauri kukosoa na kudhihaki pia
Hapa naweza kusema kuwa kuna baadhi ya vitu au mambo ulikosa kuyajua kuhusu maisha,biashara na elimu.
NB:Mwenye chake apewe
Maisha:Mkuu bado haujajiweka malengo sahihi ya maisha yako kuwa unataka uwe nani,uishi maisha ya mtindo gani na pia bado haujajingea mihimiri mahili ya mifumo ya maisha yako.Kiujumla naweza kusema bado unayumbishwa na mazingira huku sifa kama kutokujiamini,nidhamu ndogo ya kile unachofanya,huna uvumilivu wa kutoka,jealous katika kuchagua faida na hasara za kitu e.g ulisoma kitabu cha poor dad and rich dad lakini ukaona upande chanya tu wa biashara pia katika mfano wa elimu yako wakati upo huko masomoni ulikuwa unaona faida chanya tu elimu.
Biashara:Hii kitu inahitaji umakini wa hali ya juu,mkuu wewe ulikosa bussiness skills ndio maana unaona unayumba yumba.Biashara ndio msingi mkubwa wa mafanikio ya watu katika maisha unless labda unaataka kuendelea kutumikishwa katika mabiashara ya watu e.g huko shule unakoenda.
GO AND DIG DEEPER BUSSINESS SKILLS.
Elimu:Hapa mkuu ulishindwa kuitumia elimu yako ipasavyo,lakini pia elimu hiyo hiyo imekufanya ushindwe kujiamini katika uratibu wa maisha yako e.g umeamua kuanzisha biashara lakini umeficha vyeti ndani ya begi,hii inaonyesha kuwa ulishindwa kujiamini katika biashara yako ukitegemea elimu,lakini pia kama ulisoma vizuri hicho kitabu cha poor dad and rich dad kuna sehem rich dad anasema "the study of money is not at school",sasa wewe uliona hiyo elimu yako ya shule ndio msingi dhabiti wa kile unachotaka kufanya kuhusu pesa.
TOAFUTISHA KATI YA ELIMU NA ELIMU YA DARASANI
Thanks;