kesho kutwa
JF-Expert Member
- Dec 7, 2016
- 1,722
- 1,965
- Thread starter
- #21
Barabara! Sio Ile inayotumiwa kupitisha vehicles!.. Mkuu nimekupata Sana katika makala yako Kwangu!Hapa naweza kusema kuwa kuna baadhi ya vitu au mambo ulikosa kuyajua kuhusu maisha,biashara na elimu.
NB:Mwenye chake apewe
Maisha:Mkuu bado haujajiweka malengo sahihi ya maisha yako kuwa unataka uwe nani,uishi maisha ya mtindo gani na pia bado haujajingea mihimiri mahili ya mifumo ya maisha yako.Kiujumla naweza kusema bado unayumbishwa na mazingira huku sifa kama kutokujiamini,nidhamu ndogo ya kile unachofanya,huna uvumilivu wa kutoka,jealous katika kuchagua faida na hasara za kitu e.g ulisoma kitabu cha poor dad and rich dad lakini ukaona upande chanya tu wa biashara pia katika mfano wa elimu yako wakati upo huko masomoni ulikuwa unaona faida chanya tu elimu.
Biashara:Hii kitu inahitaji umakini wa hali ya juu,mkuu wewe ulikosa bussiness skills ndio maana unaona unayumba yumba.Biashara ndio msingi mkubwa wa mafanikio ya watu katika maisha unless labda unaataka kuendelea kutumikishwa katika mabiashara ya watu e.g huko shule unakoenda.
GO AND DIG DEEPER BUSSINESS SKILLS.
Elimu:Hapa mkuu ulishindwa kuitumia elimu yako ipasavyo,lakini pia elimu hiyo hiyo imekufanya ushindwe kujiamini katika uratibu wa maisha yako e.g umeamua kuanzisha biashara lakini umeficha vyeti ndani ya begi,hii inaonyesha kuwa ulishindwa kujiamini katika biashara yako ukitegemea elimu,lakini pia kama ulisoma vizuri hicho kitabu cha poor dad and rich dad kuna sehem rich dad anasema "the study of money is not at school",sasa wewe uliona hiyo elimu yako ya shule ndio msingi dhabiti wa kile unachotaka kufanya kuhusu pesa.
TOAFUTISHA KATI YA ELIMU NA ELIMU YA DARASANI
Thanks;
Maisha: Kuhusu maisha ni kweli bado sijayajua Sawa Sawa kwani miaka Toka 2001 darasa la kwanza to 2018 chuo sijaishi mtaani kiasi cha kupata unyambuliko skills kuhusu maisha.
Biashara: sijawahi fikiria hata sekunde 1 kuachana na biashara kwani najua ndio msingi mkubwa wa maisha ndio Maana nimekua nikitumia muda wangu Toka nimalize chuo kupambana na biashara, ingawa Kuna changamoto kadhaa ambazo zinapelekea nijione nimekosea na Hali ya kuto jiamini ndo imechimbuka hapo!
Elimu: nilikua nakisoma kitabu cha poor dad rich dad niliangalia upande wa advantages Sana ndio Maana nilijitutumua niingie huko kabla ya kuajiriwa! Lakini pia nilikosa kujua utofauti Kati ya elimu ya darasani na elimu ya maisha kwa ujumla wake Hali hii nayo inaniyumbisha Sana huku mtaani jambo Linafanya nifikirie tena ajira!
Mwisho kabisa Asante kwa mchango wako pia umeweka tu bayana nilivyo lakini hujanishauri lolote tafadhali kwa kutumia mantiki yako ya awali nishauri jambo mkuu
Ubarikiwe!