Hizi drama kwenye treni ya SGR nadhani zina lengo ovu

Sidhani kama kuna hujuma kwenye hili, Rais mwenyewe aliwahi kuisema adhma ya Serikali kununua vyuma chakavu na mikweche kwa kuanzia.... Tena hata sheria ya kununua vyuma chakavu ilitungwa .... Kwa vyombo vya umma huku ma VX ya viongozi yakinunuliwa mapya.... 🤔
 
Shida ipo kwenye usimamizi wa miradi. Ata wakiwekeza fedha haluna wa kuisimamia. Miradi itakufa kam DART
Shida ya usimamizi unaotengenezwa na hao hao viongozi wakijua kuwa wananufaika na ufisadi huu.... Kumbuka tangu awamu ya nne iliwahi kutungwa sheria inayo yalazimisha mashirika yote ya umma kuorodheshwa kwenye soko la hisa ili yauze hisa kwa wananchi na kupata mitaji. Miaka yote hii wanalikwepa hili.
 
Hakuna taasisi Tanzania yenye uchumi wa kuwekeza bandarini. Na pia ni uwendawazimu kuwekeza kwenye kitu kimoja, hiyo mifuko inawekeza kwenye porfolio sio kudumbukiza mayai yote kwenye kapu moja.
 
Uko sahihi kabisa. Hapo wanapanga kuwapa watu binafsi lakini wakaona watengeneze mazingira kwanza. Siku si nyingi utasikia Maushungi anasema imetushinda hivyo anapewa mwekezaji kama ilivyokuwa kwa bandari. Hizi fedha zinatumika kununua viongozi wa dini na vyama vya upinzani na kila mtu mwenye ushawishi hazitolewi bure. Ni mahesabu ya watu.
 
Hakuna taasisi Tanzania yenye uchumi wa kuwekeza bandarini. Na pia ni uwendawazimu kuwekeza kwenye kitu kimoja, hiyo mifuko inawekeza kwenye porfolio sio kudumbukiza mayai yote kwenye kapu moja.
Bandari mbona kama inasimamiwa vizuri haihitaji fedha za nje? Bandari zote za Tanzania ni mali ila kina maushungi waliwapa waarabu kwa sababu ya akili ndogo na ulafi na uvivu.
 
Hizi drama zinaonesha zitaendelea sana pasipo kubwa na kiongozi atakayeweza kusema hapana, kuna mdau aliwahi kuchangia nimesahau kuna lake akasema wamiliki wengi wa mabasi ya kutumia barabara hivi ya Morogoro road ni watu wenye vyeo serikalini alafu unaleta treni utategemea ifanye kazi ? Nilimwelewa sana mdau
 
Tokea lini mtu mweusi akaweza kusimamia na kuendesha vitu vyake...
 
Ndiyo maana nataka uhakiki thabiti kwenye hizi habari za hujuma.

Isije kuwa watu wamenunua treni chakavu mpaka wamejitungia sheria kabisa ya kufanya hivyo, halafu likibuma wanakimbilia kulaumu hujuma ambazo hata hawazielezei vizuri.
 
Hakuna taasisi Tanzania yenye uchumi wa kuwekeza bandarini. Na pia ni uwendawazimu kuwekeza kwenye kitu kimoja, hiyo mifuko inawekeza kwenye porfolio sio kudumbukiza mayai yote kwenye kapu moja.
Really? Umoja fund waliwahi kuwekeza kwenye bank ya NMB na mafanikio yalionekana, iweje washindwe kupata pesa za kuwekeza bandarini? Vipi mifuko ya NSSF, nayo haina uchumi wa kuwekeza bandarini? 🤔
 
Au ndiyo wanatafuta sababu ili wawaite tena wajomba zao waje kama kule bandarini.
 
Shida kubwa sio hujuma,bali usimamizi m'baya wa miradi ya serikali.Viongozi wetu wengi kwenye ngazi za maamuzi ni myopic,hivyo kutegemea utendaji mzuri toka kwao ni ishara ya udumavu wa akili na uwezo wa kifikra.
 
Kwani Kuna shida Gani wakija wenye fedha na kuongeza mabehewa ili kuongeza Root za Dom- moro, moro _Dar, Dom _dar?
Root ziwe nyingi zaidi.
 
Really? Umoja fund waliwahi kuwekeza kwenye bank ya NMB na mafanikio yalionekana, iweje washindwe kupata pesa za kuwekeza bandarini? Vipi mifuko ya NSSF, nayo haina uchumi wa kuwekeza bandarini? 🤔
Unahisi kwanini taasisi kama Berkshire Hathaway, investment groups au holding companies hazimiliki kampuni moja 100%. Unakuta wanagawa mitaji kwenye makampuni tofauti hata elfu moja, kwanini wasiweke kampuni kubwa moja au mbili?

Mashirika ya hifadhi ya jamii hayawezi fanya betting eti yawekeze kwenye bandari hela zote. Ikitokea tsunami investment yao yote ipotee kwa pamoja. Sheria moja kuu ya uwekezaji, kuna FAIDA na HASARA. Wewe unafanya assumption kwamba bandarini hakuwezekani kutokea hasara. Kosa hilo
 
Tukitaka kufanikiwa kuendesha hizi taasisi na mashirika ya serikali kwa ufanisi na tija ,ni lazima tuadopt ethics na professionalism ya corporate world na si umbumbumbu huu wa kuteuana kikada ili kupeana nyadhifa za uongozi na uendeshaji wa hayo mashirika .
Ikibidi turecruit hata ceo expatriates waje na team zao za baadhi ya watu ili kuongoza haya mashirika kwa miaka kadhaa ili wazawa waadopt techniques na culture ya jinsi makampuni makubwa duniani yanayojiendesha .
Na pia ccm iache usenge wa kuingilia uendeshaji wa haya mashirika , yaachiwe autonomy ya kufanya kazi
Pia mfumo wa ajira wa haya mashirika ufuate principles za merits na metrics za kupima ufanisi kama private sector vifuatwe kwa umakini mkubwa ,anayeharibu na kufanya misconduct afukuzwe kazi mara moja na si huu upuuzi wa kuhamishwa ,uje uone kama results hazijawa superb na nchi kupiga hatua .
Watu wanafanya Madudu wanajua hamna effects za kuwagusa na kuwaumiza humo serikalini na kwenye hizo taasisi na wanauhakika wa mishahara na output ni zero ,ni upuuzi sana
 
Umesahau tuliweka watu binafsi wakachukua mabehewa na kufumua reli na ili kuenda kuuza hukokwao chuma chakavu? Reli ya kuelekea tanga na arusha huyo alipanga kuifumua. Usisahau na ATC ilivyotelekezwa na pia TANESCO. SIO VITU VYOTE VINABINAFSISHWA. HATA ULAYA MFANO BRITSH RAILWAY, AIRWAYS, SWISS AIR, KLM bado ni mali ya serikali . Fikiria zaidi. Hakuna wa kutujengea nchi zaidi sisi wenyewe.
 
Ninafahamu hayo uliyosema, hata hivyo sijasema kubinafsisha yaani kugawanya umiliki au kubadilisha umiliki, ninachoshauri ni kuachia sekta binafsi kazi za kuiendesha TRC, ku-sub contract baadhi ya kazi km ulinzi, kukata tiketi, vinywaji ndani ya treni..nk ili serikali ibaki na jukumu la kusimamia na kulinda miundombinu iliyoijenga..
 
Ushindani huleta ubora wa huduma..mabasi yatakuwepo tu km huduma zao zitavutia abiria na treni itakuwepo pia..! vyote vinategemeana! in everything there must be an alternative!
 
Ni Abdul mtoto wa kiume wa chura kiziwi wa kizimkazi anataka kuwekeza na Rostam Aziz. Ikumbukwe hawa wamekuwa marafki wakubwa na Abdul anaishi jumba la kifahari Dubai alilopewa bure na kampuni ya DP WORLD iliyopewa bure bandari yetu
 
Shida ipo kwenye usimamizi wa miradi. Ata wakiwekeza fedha haluna wa kuisimamia. Miradi itakufa kam DART
una maana gani kusema hakuna wa kusimamia? hawapo wenye sifa kusimamia au uwezo? lkn kuwa na hisa si lazima uwe msimamizi wa mradi, mashirika yanaendeshwa kwa utaratibu ambao wanahisa wanataka, wakipendekeza MD apatikane kwa usaili na kwa ushindani..basi inakuwa hivyo..
 
Hakuna taasisi Tanzania yenye uchumi wa kuwekeza bandarini. Na pia ni uwendawazimu kuwekeza kwenye kitu kimoja, hiyo mifuko inawekeza kwenye porfolio sio kudumbukiza mayai yote kwenye kapu moja.
Huko wanakotumbukiza kwenye portfolio wanapata nini?? mbona hata kulipa mafao wenye hela zao walioweka wanashindwa? mfano, hizo nyumba za kigamboni zinawapa nini NSSF kwa sasa..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…