Crocodiletooth
JF-Expert Member
- Oct 28, 2012
- 20,561
- 24,428
Mkurugenzi wa TRC asimame imara, atajijengea heshima kubwa kabisa kwa mradi kama huu kusimama imara na kuonyesha dalili zote za kuingiza faida kubwa, tunafahamu wapo ambao hili wanaliona kwao ni hapana na wangependa mapato haya manono wayaingize mfukoni mwao, umefika wakati baada ya uwekezaji mkubwa TRC nayo ikatoa gawio nono la kustaajabisha kwa serekali yetu, wapo wengi kwa ulafi wao wanautamani mradi huu uwe wao, aidha serekali iwakodishe washenzi hao, badala ya mradi huu kusimamiwa na serekali yetu, tuwe imara tusichotwe mawazo, MAPUMBAVU yasiunase mradi huu kamwe!Kwa muda sasa kumekuwa na shutuma kuhusu hujuma inayohusu treni ya SGR, tukumbuke huko nyuma kuliwahi kutolewa wazo la kuruhusu watu binafsi waweke vichwa na mabehewa yao kwenye huo mradi,
Wazo ambalo lilikuja mapema sana hata kabla treni hazijaanza kufanya kazi!
Nikiangalia tuhuma hizi za sasa naona kama zinatengenezwa ili ziwe kichocheo cha ajenda ya kuwa ili kuboresha ufanisi serikali iruhusu watu binafsi waingize injini na mabehewa yao kwenye SGR, tujiulize watu hao wanaopigiwa debe kabla ya wao kuomba ni akina nani?
Mimi ninadhani ni kati ya waliokuwa wanakwenda huko zilikotoka injini na mabehewa ya SGR, na je, wataleta mapya yapambane na haya yanayodaiwa kuwa ni mitumba?
Hebu tungoje kwani muda utajibu kitendawili hiki.
The end of the beginning.