Hizi drama kwenye treni ya SGR nadhani zina lengo ovu

Mkurugenzi wa TRC asimame imara, atajijengea heshima kubwa kabisa kwa mradi kama huu kusimama imara na kuonyesha dalili zote za kuingiza faida kubwa, tunafahamu wapo ambao hili wanaliona kwao ni hapana na wangependa mapato haya manono wayaingize mfukoni mwao, umefika wakati baada ya uwekezaji mkubwa TRC nayo ikatoa gawio nono la kustaajabisha kwa serekali yetu, wapo wengi kwa ulafi wao wanautamani mradi huu uwe wao, aidha serekali iwakodishe washenzi hao, badala ya mradi huu kusimamiwa na serekali yetu, tuwe imara tusichotwe mawazo, MAPUMBAVU yasiunase mradi huu kamwe!
 
Samia kwa uanamke wake ameshafanya mengi sana ambayo wanaume watano waliyashindwa, huwezi ukayaona kwa sababu kichwani umeshatanguliza udhaifu wa kumtazama na kumhukumu kwa uanamke wake.

Kabla yake alikuwa mwanaume ambaye baadhi yetu walifanya sherehe siku kifo chake kilipotangazwa kwa umma, unajua kwanini kwa hao watu ilikuwa ni siku ya furaha?.
 
Huwezi ukaachia makampuni binafsi miradi kama hii nyeti ya kiuchumi.

Lazima "mkono" wa serikali uwepo.
 
KInachokoseka ni msimamizi mwenye uzalendo na uchu na mradi, visionary na mwenye jicho la kuona both long and short term of the project. Ili mirafi iwe endelevu even if it means working outside the books.
Ila sio hii ya kununu hisa na kupewa isimamizi wa mradi wanachofanya ni kutafta profit kwa walichokiweka.

Mfano TTCl wawekezaji walipata profit na kuondoka na chao. Pesa ilikuwepo ila Kilichokosekana ni mtu mwenye maono na kusamia miradi iwe endelevu isife. Ni bora mradi apewe mtu wa private sector au simamie atakua na uchungu nao kuliko shirika la serkali.
 
Private sector dunia nzima inaendeshwa kinyapara na results zinaonekana ,hii lazyfair ya serikali ni upuuzi ,bila mabadiriko ya kweli ya kimfumo kila siku kilio kitakuwa ni kile kile tu.
Ni sawa na kujenga ghorofa zuri kwenye msingi wa tofali za tope ,work done =zero
 
Huwezi ukaachia makampuni binafsi miradi kama hii nyeti ya kiuchumi.

Lazima "mkono" wa serikali uwepo.
Halafu usipotoshe kusema UKAACHIA..sina maana hiyo, mfano wanaochimba madini migodini ni serikali?? au madini si miradi nyeti kwa maana yako..? kwa maana ya kuwa na ufanisi serikali ielekeze nguvu nyingi kwenye kulinda na kusimamia miundombinu, mambo ya uendeshaji baadhi ya kazi wa-sub contract sekta binafsi, serikali hawana uwezo wa kubeba majukumu yote kwa utimilifu!
 
Hakuna aliyesema kuwa ni lazima wawekeze kwenye bandari pekee ni kwamba wanayo nafasi ya kuwekeza sehemu mbali mbali zinazo lipa kwa mtindo ule ule wa mgawanyo wa portfolio walizochagua.
 
Ni wanaccm ndiyo wanafanya huo upumbavu
 
Wazo la kununua vichwa mtumba lilikuwa la kijinga sana, sijui tuliwaza nini. Mwendokasi inavotupeleka puta nahofia yasije kufikia kwenye mradi wa maana na mzuri kama huu
Matrioni ya fedha za umma yamepigwa na mafisadi ya CCM
 
Hakuna aliyesema kuwa ni lazima wawekeze kwenye bandari pekee ni kamba wanayo nafasi ya kuwekeza sehemu mbali mbali zinazo lipa kwa mtindo ule ule wa mgawanyo wa portfolio walizochagua.
Kuhusu portfolio nakubali ila kwa umakini mkubwa mno. Kuna sababu kwanini mashirika mengi ya hifadhi ya jamii duniani huwa hayawekezi, mifumo mingi imejaribiwa na ikachukuliwa iliyo safe zaidi.

Shirika la hifadhi ya jamii hata lisipopata faida ni sawa, kazi yake kubwa lisipate hasara maana litaua vibaya sana uchumi wa nchi.
 
Huko wanakotumbukiza kwenye portfolio wanapata nini?? mbona hata kulipa mafao wenye hela zao walioweka wanashindwa? mfano, hizo nyumba za kigamboni zinawapa nini NSSF kwa sasa..
Sasa walioshindwa kwenye portfolio ndio wataweza kwa kuwekeza kitu kimoja?

Wasomi uchwara haohao wameshindwa kupata hela kwenye uwekezaji wa manyumba ambao hata vilaza wasiojua kusoma na kuandika wakiotea hela wanajenga na kupangisha na kupata faida. Watu haohao mnataka wawekeze kwenye bandari ambayo ni ngumu sana kuliko kuendesha na tangu tupate uhuru haijawahi kuwa efficient?
 
Labda hujaelewa toka mwanzo, uwekezaji tunaosema ni wa mifuko ya jamii kutumia pesa za wanachama kununua hisa kwenye kampuni zilizowekeza miradi mikubwa hapa ndani km zile za madini au kwenye usafirishaji..hata bandari pia km inawekwa kwenye soko la hisa ili watanzania washiriki kumiliki na kuendesha uchumi kwa faida yao..
 

Alichokisema Mkurugenzi. Mkurugenzi TRC: Tutaruhusu Wawekezaji binafsi kwenye Mradi wa SGR kuingiza Vichwa vya Treni na mabehewa yao.​

 
Unamwamini atakayevifungua hivyo vibox?
 
Hawa Trc hawako serious kabisa mimi juzi nilibooking tickets ya jumapili nikatumiwa control no nikafanya malipo nikabaki na sms ya muamala na Tickets no jumapili imefika nakwenda kituoni naonyesha Ticket yangu naambiwa haitambuliki mara sijui ilicanceliwa kitu ambacho kama wangecancel wangerudisha mesej ya muamala nilipandwa na hasira sana
 
Usiamini biashara ya booking, kama unania ya kusafiri kata tikiti yako kwa kuilipia kabisa, kuhusu hilo lako mwenye pesa mkononi ndiye anathiniwa.
 
Unaweza kutuonyesha huyo serikali?
Kama una muondoa kadogosa
 
kwakweli wabongo wa ajabu sana ntu anapanda treni na sanduku sijui limebeba spear za howo? zito kweli hadi sehemu za kuwekea mabegi zinapinda, ipo haja ya kuwela limit ya kg za kubeba, lia ziletwe behewa zenye booty kama kilimanjaro express mabegi yawekwe huko

kuhusu kudhibiti mifuko ya rambo na watu kupanda na makande hongera sana, kwakweli hali ya usafi ni ya hali ga juu sana
 
Tanzania ndo nchi pekee ukiwa tajiri ni km laana maana kila sku matajiri wanaonekana wabay

Baba yangu aliwai kunambia neno moja Wenye Nyumba za nyasi wao huwa hawaonei ? wao kila sku wanaonewa ! na hii ilitokana. Kuna wanakijiji walijenga nyumba kwenye viwanja vya mzee sasa pind anashugulika kurudisha maeneo yake ndo akasema ivyo

Maskini wao kila sku wanaonewa wao huwa hawaonei

Tupunguze majungu na vijimaneno maneno visivyo na maana huu mradi ni mpya na inawezekana bado mamlaka ya usimamizi haijajua vzr jinsi ya kupambana na kuepuka changamoto wanazokutana nazo kwa sasa tuwape muda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…