Kenya 2022 Hizi hapa sababu za kuchelewa matokeo ya Urais Kenya

Kenya 2022 General Election

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC imetoa ufafanuzi kuhusu sababu za kuchelewa kutoa Matokeo pamoja masuala mengine yanayolalamikiwa na hatua inazochukua

Tume imesema kwasasa inafanyia kazi masuala yafuatayo:-

1. Uthibitishaji wa picha ya Matokeo ya Fomu 34A dhidi ya Fomu 34B
2. Uthibitishaji wa Fomu za 34A za eneo bunge dhidi ya Fomu asili za 34A.
Fomu 34A zilizothibitishwa zinalinganishwa na Fomu halisi 34B, ambazo pia huwasilishwa na Msimamizi wa Uchaguzi wa Kaunti (CRO's).
CROs walitakiwa kuwasilisha fomu mbili kwenye Kituo cha Taifa cha Kuhesabu kura: Fomu 34A na 34B.
Tume kwa sasa iko katika hatua hii na tayari imehakiki Fomu 133, ikilinganishwa na idadi ya majimbo yote yaliyopiga kura.
Hata hivyo, baadhi ya Wasimamizi wa Uchaguzi bado hawajafika eneo hilo kuwasilisha nyaraka zao kwa ajili ya kufanyiwa kazi.
3. Kuunganishwa kwa Fomu 34C na uthibitisho wa Mshindi wa Urais kwa kiwango cha Kikatiba cha 50% pamoja na Kura moja na 25% ya Kura za kaunti.
Fomu 34B sasa zitaunganishwa kuwa hati moja, na hivyo kuunda Fomu 34C.
Tume hiyo itathibitisha ni nani amepata 50% inayohitajika pamoja na 1% ili kumpata mshindi wa Urais.
4. Kutangaza Matokeo ya Urais
Baada ya Mgombe anayeongoza kutambuliwa, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Wafula Chebukati, atamtangaza Mshindi Rasmi.
5. Kutolewa kwa Cheti kwa Rais Mteule.
Mshindi wa Kiti cha Urais atakabidhiwa Cheti cha uthibitisho wa Ushindi wake kutoka Tume ya Uchaguzi.
Haya yote lazima yafanyike kabla ya siku ya mwisho Kikatiba ambayo ni Jumanne ya August 16, 2022. Katiba ya Kenya inatoa siku 7 kwa Tume kutangaza matokeo ya Urais kuanzia siku ya kupiga kura.

Source: Citizen Digital
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…