Hizi hapa taasisi zilizorudisha rushwa kwa kasi ya ajabu awamu ya sita

Hizi hapa taasisi zilizorudisha rushwa kwa kasi ya ajabu awamu ya sita

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
1. Jeshi la Polisi - trafic na CID wanakula vitu vinono. Kila kona ya nchi kuna trafic na wapo radhi kusimama akusanye buku buku akifika jioni apeleke nyama home. Uchunguzi hasa case za kuibiwa vifaa vya electroni hakuna anayechunguza. Mtaani panejaa simu na computer za wizi. Watu wa cyber wapo tu na hivi vifaa ndivyo vinatumika kwenye uhalifu. Rushwa imeifanya nchi iwe damping ya vifaa vya wizi. Watu wanakufa kwa kushambuliwa na wezi au majambazi ila no serious investigation

2. Mahakama: kama Kawa wataalam wanajiita miungu wa Duniani. Karani wa mahakama ana nguvu ya kufuta kesi kabla hakimu au judge ataandika hukumu. Makarani ni viungo wachezaji kwenye game ya kitu kidogo

3. Ofisi ya DPP- hapa anayefikishwa mahakamani ni yule asiye na pesa. Kama una salio jalada lako litaishia mikononi mwa watendaji wa mwamba huyu.

4. Halmashauri - kupitia Tozo mingi watendaji wote wa halmashauri wamegeuka wakusanya mapato kwa opereshini bubu. Wamegoma wafanyabiashara kutumia mifumo ya electronic kupata leseni na kukamilisha huduma bila kwenda ofisini

5. TRA- kodi zimekuwa nyingi na wateja wanasumbuliwa kwa kubambikiwa kodi kuanzia bandarini na sokoni. Wanapitisha mizigo ya magendo mipakani

6. Uhamiaji na Pasipoti; wateja kwa sasa wanasubiri pasipoti mwezi mmoja. Vinginevyo ukate mpunga kwa vishoka waliopo nje ya ofisi zao. Hakuna anayejali uliomba pasipoti lini

7. Hospitali uchakachuaji wa huduma za bima na kuruhusu bima kutumika kinyume cha taratibu

8. Idara za maji- kuunganisha maji na ubambikiaji bills

9. Ardhi eneo la utoaji hati na umilikaji ardhi

10. NIDA kwenye uandikishaji na utoaji kadi
 
Kwani ni lini rushwa imeondoka huko kote?

Mbona ipo miaka yote.

Kungekua hamna rushwa tungekua tumepiga hatua kubwa sana.

Rushwa ni adui mkubwa sana.

Madhara ya rushwa ni makubwa sana ni vile tu watu hawajui.

Chochote kibaya unachokiona hapa Tanzania chanzo chake ni rushwa.
 
1. Jeshi la Polisi - trafic na CID wanakula vitu vinono. Kila kona ya nchi kuna trafic na wapo radhi kusimama akusanye buku buku akifika jioni apeleke nyama home...
Kwakweli trafic ni haibu kubwa sasa hv yani rushwa ni njenje
 
Nchi hii rushwa ipo na itaendelea kuwepo

Ova
 
1. Jeshi la Polisi - trafic na CID wanakula vitu vinono. Kila kona ya nchi kuna trafic na wapo radhi kusimama akusanye buku buku akifika jioni apeleke nyama home....
JPM alitumia mazingira ya rushwa ya juu (grand corruption) akahamisha fedha ya kujenga uwanja wa ndege wa Kajunguti bukoba hadi Chato. Ndege ya Precision kutumbukia ziwa victoria mwaka jana ilichangiwa na uwanja hafifu uliopo kwenye hali mbovu ya hewa.
 
Kuhusu vibaka mbezi malamba mawili saa 3 tu usiku vibaka wanavamia nyumba na kupora,hivi vitendo vilishasahaulika ila vimerudi kwa kasi mno!
 
Umeandika matatizo yanayojulikana bila kutowa ushauri wa nini kifanyike kuondowa tatizo. Niliandika na kushauri hivi:


Mbona wakati wa JPM yalipungua,shida ipo kwa na hili mkalitazame
 
1. Jeshi la Polisi - trafic na CID wanakula vitu vinono. Kila kona ya nchi kuna trafic na wapo radhi kusimama akusanye buku buku akifika jioni apeleke nyama home. Uchunguzi hasa ...
WIZi WA Mtandaoni umezidi. MTU anaamka anafungua Instagram page anatangaza business. Tunalipia Kwa Bank, Simu.

Wanaondoka hwani wameshaliza Watu. Ukiripoti Cyber Crime hawafanyi lolote zaidi ya kuaminishwa watafuatilia. Anyway unachotafuta unaweza kukilipia Rushwa na usikipate. Business as Usual.
 
Back
Top Bottom