Hizi hapa taasisi zilizorudisha rushwa kwa kasi ya ajabu awamu ya sita

Hizi hapa taasisi zilizorudisha rushwa kwa kasi ya ajabu awamu ya sita

Magufuli alisema rushwa ya traffic ni ela ya kupiga viatu rangi. Au ushasahau?
Bora ya hao tubukubuku, buku mbili mpaka buku tano haziumizi ingawa anakusanya kwa wengi na anapata nyingi kwa siku. Kuna watu wanapiga rushwa mishindo mpaka unajiuliza huyu ana akili kweli?!

T.R.A huko mtu anataka umpe laki tano mpaka milioni na zaidi, Bandari, uhamiaji na wizara zinginezo... hao ndo wala rushwa nguli

Hao matrafiki kwa kweli wana maisha magumu wacha wajikusanyie vitakasa nafsi ingawa wapunguze kidogo
 
Rushwa ipo popote wakati wowote, tena kipindi chake ndio watu wanalikua wanapiga ela kimya kimya bila kelele yeye akiwa kinara wao, maana vyanzo vya kutoa habari vilikua vimebanwa, mtu ukitoa taarifa ya rushwa unatafutwa wewe, ukitoa taarifa ya mradi m'bovu unakamatwa wewe, nadhani mnakumbuka alietoa taarifa ya ubora wa majengo ya mlimani cuty kilichomkuta

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walishaagizwa kuwa wale rushwa na kufanya ufisadi
 
Awamu dhaifu, mama anaupiga mwingi hadi kwenye matope!.
Awamu ya 4 (JK) = Awamu ya 6 (Sa100)

Allahu akbar,Mungu aepushie mbali fikra za watu wa hovyo kama hizi,leo mnatamani kweli yule Jamaa angekuwapo madarakani??

Ni watu wenye roho ngumu kama za waana wa israel watanzania
 
Kuhusu vibaka mbezi malamba mawili saa 3 tu usiku vibaka wanavamia nyumba na kupora,hivi vitendo vilishasahaulika ila vimerudi kwa kasi mno!
Tuweke ulinzi shirikishi maana polisi walikuwa wanajitahidi sana kutupatia huduma ya ulinzi ila Watz tulivyomafala hatuthamini kwamba wenzetu(polisi) wanahatarisha maisha yao kwa ujira mdogo,sasa mwishowe ndio kama hivi mapolisi wanatususia kiaina ili tuonje joto la jiwe. Huku mtaani mali zetu na uhai wetu havipo salama.
 
1. Jeshi la Polisi - trafic na CID wanakula vitu vinono. Kila kona ya nchi kuna trafic na wapo radhi kusimama akusanye buku buku akifika jioni apeleke nyama home. Uchunguzi hasa case za kuibiwa vifaa vya electroni hakuna anayechunguza. Mtaani panejaa simu na computer za wizi. Watu wa cyber wapo tu na hivi vifaa ndivyo vinatumika kwenye uhalifu. Rushwa imeifanya nchi iwe damping ya vifaa vya wizi. Watu wanakufa kwa kushambuliwa na wezi au majambazi ila no serious investigation

2. Mahakama: kama Kawa wataalam wanajiita miungu wa Duniani. Karani wa mahakama ana nguvu ya kufuta kesi kabla hakimu au judge ataandika hukumu. Makarani ni viungo wachezaji kwenye game ya kitu kidogo

3. Ofisi ya DPP- hapa anayefikishwa mahakamani ni yule asiye na pesa. Kama una salio jalada lako litaishia mikononi mwa watendaji wa mwamba huyu.

4. Halmashauri - kupitia Tozo mingi watendaji wote wa halmashauri wamegeuka wakusanya mapato kwa opereshini bubu. Wamegoma wafanyabiashara kutumia mifumo ya electronic kupata leseni na kukamilisha huduma bila kwenda ofisini

5. TRA- kodi zimekuwa nyingi na wateja wanasumbuliwa kwa kubambikiwa kodi kuanzia bandarini na sokoni. Wanapitisha mizigo ya magendo mipakani

6. Uhamiaji na Pasipoti; wateja kwa sasa wanasubiri pasipoti mwezi mmoja. Vinginevyo ukate mpunga kwa vishoka waliopo nje ya ofisi zao. Hakuna anayejali uliomba pasipoti lini

7. Hospitali uchakachuaji wa huduma za bima na kuruhusu bima kutumika kinyume cha taratibu

8. Idara za maji- kuunganisha maji na ubambikiaji bills

9. Ardhi eneo la utoaji hati na umilikaji ardhi

10. NIDA kwenye uandikishaji na utoaji kadi
Ukiwa summoned na Mamlaka husika unaweza kuthibitisha haya?

Pili Kati ya Samia na Mwendazake nani aliwaruhusu Polisi kula Rushwa?

Kati ya Samia na Mwendazake nani amekuwa anaitaka Mahakama kutenda Haki?

Mwisho kama kote huko Kuna Rushwa inakuaje Serikali awamu hii Ina mapato mara 2 ya mapato ya Mwendazake?
 
Back
Top Bottom