Hizi kampeni za Valentine's Day katika media za Tanzania zina tija gani kwa maendeleo ya Watanzania?

Hizi kampeni za Valentine's Day katika media za Tanzania zina tija gani kwa maendeleo ya Watanzania?

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Wiki hii kila ukifungulia tu Redio yoyote cha Kwanza utakachokutana nacho ni mambo ya Mahaba hasa kuelekea Siku ya Wapendanao (Valentine Day).

Je, ina maana Media za Tanzania zinashindwa pia kwa Umoja wao huu huu (Media Agenda) basi wakawa Wanayasema yale ya Ukweli kuhusu Maisha ya Mtanzania, Demokrasia ya Tanzania na Kukosoa Mapungufu ya Watawala (Serikali) husika?

Au Akilini mwa Watanzania wengi ni Mambo ya Kupendana na Ngono tu pekee?
 
Huwezi amini sijasikiliza redio nina miaka. Labda itokee bahati mbaya mtu kawasha kwenye daladala au nyumbani kwake.
 
Kwenye television pia mfano wale dadaz eti kila wakati yanaoneshwa na migauni yao utadhani mashetani halafu yamenyataa!!!
 
Fungua redio yako ueleze mambo ya maendeleo muda wote sio kupangia ofisi za watu sio taasisi za umma hizo watu wameweka pesa zao.
 
Wanafanya kwa ajiri ya faida yao,washajua wabongo wanapenda sana ngono na wao wanawapeleka mule mule.
 
Hoja ya msingi sana hii mkuu, yaani media zinatumia nguvu nyingi sana kwa mambo ya kijinga kabisa. Huwezi hata siku moja kusikia wakiungana kujadili changamoto Muhimu za kitaifa kama gonjwa lililopo hivi sasa, na mengine mengi tuu...
 
Hii agenda ilianzishwa na clouds media wakina marehemu Ruge ndiyo walikuwa vinara wa hiyo ishu.
 
Kwenye television pia mfano wale dadaz eti kila wakati yanaoneshwa na migauni yao utadhani mashetani halafu yamenyataa!!!
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Siwapendi kweli kweli, yaani kipindi hovyo kabisa..
 
Hoja ya msingi sana hii mkuu, yaani media zinatumia nguvu nyingi sana kwa mambo ya kijinga kabisa. Huwezi hata siku moja kusikia wakiungana kujadili changamoto Muhimu za kitaifa kama gonjwa lililopo hivi sasa, na mengine mengi tuu...
mambo ya kijinga ndio yana hela
 
Mkuu siyo kwamba hawataki kuyasema ila wanaogopa rungu la TCRA, maana ukiachilia mbali kuwa ni media, wamiliki wamezianzisha Kama njia ya kujikwamua
 
Mbona mnafanya maisha magumu hivyo kwa hiyo muda wote wazungumzie maendeleo tu? Kuna vitu vyingi vya kuzungumza mahaba yakiwa kimoja wapo.
 
Mbona wazungu wanafanya mambo ya kijinga lkn wanahela kushinda sisi?

Kwahiyo watu wasiongelee mapenzi, wasiongee kuhusu kwenda kula bia?

Mambo yote ni ya muhimu na ya msingi. Niache kutoka na demu wangu valentine day, niongee kuhusu serikali yako halafu mwisho wa siku wanitundulisu.

Kosoa mwenyewe

Back
Top Bottom