Hizi kampeni za Valentine's Day katika media za Tanzania zina tija gani kwa maendeleo ya Watanzania?

Hizi kampeni za Valentine's Day katika media za Tanzania zina tija gani kwa maendeleo ya Watanzania?

Hayo maendeleo ndiyo unayaona leo? Tangu 1961 mpaka leo kuna vijiji havina maji, umeme na wanafunzi wanakaa chini. Hayo maendeleo unayoyazungumzia yakoje? Watu waache kufanya starehe kwasababu ya maendeleo. Familia yangu ikila na kunywa inatosha.
 
Jaribu na wewe kukosoa serikali uone mwisho wako.

Ingia hata vijijini kwenye shule ambazo hazina madawati au walimu kisha piga picha na uchukue video halafu rusha kwenye social media uone itakavyo kutokea puani.

Vitu vya msingi ni kuongea kuhusu maendeleo? Hata kunywa bia ni jambo la msingi pia.

Hoja ya msingi sana hii mkuu, yaani media zinatumia nguvu nyingi sana kwa mambo ya kijinga kabisa. Huwezi hata siku moja kusikia wakiungana kujadili changamoto Muhimu za kitaifa kama gonjwa lililopo hivi sasa, na mengine mengi tu.
 
Wiki hii kila ukifungulia tu Redio yoyote cha Kwanza utakachokutana nacho ni mambo ya Mahaba hasa kuelekea Siku ya Wapendanao ( Valentine Day )

Je, ina maana Media za Tanzania zinashindwa pia kwa Umoja wao huu huu (Media Agenda) basi wakawa Wanayasema yale ya Ukweli kuhusu Maisha ya Mtanzania, Demokrasia ya Tanzania na Kukosoa Mapungufu ya Watawala (Serikali) husika?

Au Akilini mwa Watanzania wengi ni Mambo ya Kupendana na Ngono tu pekee?
Wakitangaza serious issues hakuna atayesikiliza, watanzania wanapenda kusikiliza mambo kama hayo unayosikia kwenye hizo Radio

Sikiliza hata wasanii wa muziki wa sasa, wanachoimba ni kuhusu ngono pekee, ndio tu mambo ambayo idadi kubwa ya watu wanapenda kuona na kusikia

Tunaishi katika dunia ya ajabu zama hizi
 
Back
Top Bottom