Hizi kampuni DSE walizoshika hawa jamaa zetu dividend ni kilio

Hisa za Crdb hushuka mpaka tsh 150 kwa hisa, 150 zidisha lak 1 ni milioni 15. Si milion 200.
Bado hata ikiwa 15m halafu utegemee faida 1m kwa mwaka ni hasara kubwa. Labda kama una pesa isiyo na kazi
 
Uwekezi 200m upate faida 1m kwa mwaka tena kabla ya kukatwa kodi, kama si wendawazimu huu basi bora uitwe wehu.

Na washawasha!

Sio kweli hisa ya crdb ni kama 185 hivyo kwa 200m unapata zaidi ya hisa 1m kwa gawio la 10 unapata zaidi ya 10m. Ukumbuke gawio ni kila mwaka na miaka mingine inakuwa kubwa kutokana na faida. Sera za serikali zinachnagia faida kushuka katika mabenki. Angalau wao wanatoa kila mwaka kuna ambao hawajawahi kutoa gawio.
 
Bado hata ikiwa 15m halafu utegemee faida 1m kwa mwaka ni hasara kubwa. Labda kama una pesa isiyo na kazi

Hii ni paasive income ya investmwnt ambayo wewe hushuliki haiwezi kuwa na return sawa sawa na mfanyabiashara anaechukua risk kubwa na kushughulika masaa yote. Kingine mtaji wako upo pale pale ni longterm investment sio quick schemes
 
Bora hata hao Crdb wanatoa sh10 maana kama una hisa laki 1 unakamata milioni kabla ya kodi, kampuni nyingine toka ziuze hisa kila mwaka hasara tu, tunabaki na matumaini ya siku moja watagawa hata sh 5.
Sijui gharama ya hisa moja ya CRDB, ila niki-assume hisa moja ni sh. 250 ina maana mtu mwenye hisa laki 1 amewekeza mtaji wa sh 250 million! Sasa jiulize return ya milion moja kwa mtu mtu mwenye mtaji wa milion 250 ni biashara hiyo au kupoteza hela?

Unakuta mtu ana mtaji wa mili 2 tu anaanzisha duka la rejareja na kupata laki 3 kila mwezi sawa na sh mil 3.6 kwa mwaka zaidi ya aliyewekeza 25 mil CRDB kwenye soko la hisa
 
Wakuu mimi huwa siielewi vzuri biashara ya hisa. Mti ambaye anaifahamu vzuri anisaidie labda inaweza nisaidia nikiwekeza huko.
 
250 × 100,000 = 250,000,000/ .. hii calculation ni ya sayari gan??
 
250 × 100,000 = 250,000,000/ .. hii calculation ni ya sayari gan??
Tumechukulia mtu mwenye hisa 100,000 na tuka-assume hisa moja ina value ya 250. Ili kupata mtaji uliwekezwa na mtu huyo ni kuchukua kiwango cha hisa mara thamani ya kila hisa in our case ni 250 x 100,000.

Sasa assume kila hisa mtu anapata devidend ya 10 TSH, hii ina maana mtu mwenye hisa lak 1 atakuwa na gawio la 1M TSH.

Labda nielekeze mahesabu hapo yana shida wapi?
 
DSE Kama inataka kurutubisha hilo soko lao walazimishe makampuni yalipe dividend kila muhula.
Hii haitasaidia sana kutokana na ukweli kuwa dividend inatokana na faida? Swali ni kuwa je hali ya uchumi iliyopo je hayo makampuni yanapata faida?
 
mimi ndo maana na cheza share za online na mda huo huo na wakati huo.mpunga unacheza
 
Hisa kwa kusubiria gawio inakuwa hupati faida kwa haraka , kama unataka kupata kwa faida kwa haraki kwa kununua na kuuza hisa kwa mfano hisa za acacia alhamis zilikuwa 8,180 , ijumaa zimefika 8,500 . Sasa kwa mtu mwenye fedha za kutosha anunua tu tuseme hisa elfu kumi alhamis , ijumaa anaziuza tayari ana kama milioni tatu ndani ya masaa, machache, sasa hapo ni wewe ni kufanya calculations vizuri upige hela ndefu zaidi
 

Attachments

  • jf.JPG
    9.2 KB · Views: 30
Duuh!! Kwa mfano hisa moja inauzwa sh 500, nikiwa na sh laki tano ntanunua hisa 1000, ikiwa kila hisa napata faida( divident) sh 10, then nitakuwa na faida ya sh 10 ×1000 sawa na Tsh 10,000 kwa mwaka.
Hii biashara anaweza kufanya kichaa
Kweli aise[emoji2]
 
Hili la hisa kwa tz ni kampuni chache sana ambazo zinafanya hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…