Hizi kero ambazo NMB bank inawapa wateja wake?, ni nani anapaswa kuwajibika?

Hizi kero ambazo NMB bank inawapa wateja wake?, ni nani anapaswa kuwajibika?

Balqior

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2021
Posts
3,490
Reaction score
10,749
Habari,

Inaenda wiki sasa huduma za miamala bado hazijatengamaa kwenye swala la kutuma na kupokea hela, unaeza ukatuma hela ikaishia hewani, unaeza ukatumiwa hela ikaishia hewani.

Wengine ATM zina shida, mwingine hawezi lipia control number, wafanyabiashara wengine wanashindwa lipa suppliers wao.

Kila siku transactions za mabilioni ya shillingi zinafeli, uaminifu unapungua.

Hakuna taarifa yoyote toka kwa NMB inayoeleza kwamba maboresho hayo yatakamilika lini.

Hawa watu wapo serious kweli?
 
Nilidhani ni ushamba wangu. Kidogo nionekane tapeli ka Wakala
 
Hivi ni National Microfinance Bank ( NMB) ama NMB Bank?
 
Nlikuwa nalipia maji,
Mara naambiwa gari hili halina deni kwa sasa
 
Back
Top Bottom