Hizi kura za Dkt. Ndugulile zinaashiria Nini?


..Dr.Ndugulile ni Mkurugenzi wa WHO-Africa.

..Je, kura mnazoziona hapo sio kura za nchi za AFRIKA?

..Kupata hiyo nafasi kunahitaji mhusika awe mahiri, na pia serikali yake ifanye ushawishi wa kidiplomasia ili aungwe mkono na nchi nyingine.

..Sasa Tanzania ni mwanachama wa EAC, na SADC, kwa hiyo jumuiya hizo ni baadhi ya eneo tunakoweza kushawishi ili mgombea wetu apate kura.

..Hata Tanzania huko nyuma inaweza kuwa iliunga mkono mgombea toka nchi fulani hivyo na wenyewe wametulipa fadhila wakati huu.

..Mashirika kama WHO yana nafasi mbalimbali za kazi zenye michakato tofauti. Kuna nafasi nyingine nyingi hazihitaji mhusika kupigiwa kura na nchi wanachama wa shirika.
 
Huu ndio ukweli inaonekana muhusika alitema madini haswa Kisha baadae akaja boss wake ndugu yetu dada yetu na mama yetu Jesca
Hapana. Sio Tanzania iliyochaguliwa bali Dr. Ndugulile. Kuchaguliwa ilitegemea zaidi candidates walivyojipresent kwa delegates. Mengine campaigns & lobbying ni ziada. Unadhani ingekuwa kina mwijaku tungeambulia kitu?
 
Lucas Mwashambwa Tlaatlaah na ChoiceVariable wanajua kwa kinagaubaga......

Watuelezee tububujikwe machozi ya furaha.
ni muhimu sana shukrani zote za kipekee zimfikie Kipenzi cha waTanzania wote Dr.Samia Suluhu Hassan kwasabb ni dhahiri ushawishi wake kimataifa imefanya Tanzania kuaminika na kukubalika sana Africa na duniani kote...

influence na endorsement ya Rais Samia kwa Dr Tulia Ackson kule IPU, Dr.Faustine kule WHO na sasa hivi Raila Amolo odinga kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Africa AUC, ni dhahiri siasa za kitaifa na kimataifa ziko rohoni na mikononi mwake....

na kwa Neema na Baraka za Mungu, ni yeye tu Dr Samia suluhu Hassan kuamua cha kufanya kwasabu uwezo anao, nia anayo na kibali cha Mungu pia anacho 🐒

au nasema urongo ndrugu zango?
 
Tuambiwe ni mabilioni mangapi yametumika kumwezesha Ndugu ashinde na tutafaidika vipi na ushindi huu.
 
Positive impact ya Simba sports club kuitangaza nchi kimataifa nalisema hili bila tashwishwi wala kumung'unya maneno
In profesa wa majalalani VOICE
 
Wale walioipenda Rwanda wote waliiunga mkono Tanzania isipokuwa mmoja alienda senegal. Mmoja aliyeipenda niger round ya mwisho alienda Senegal
 
Kagame ni mbishi alitaka kutikisa kiberiti kupimana uwezo wa ushawishi na Tanzania. Jibu kashalipata.
Mbona ilikua mbinu nzuri tu.....maana kura nyingi zilizopigwa kwa Rwanda walipotoka ndo zikaipa ushindi Tanzania,,,,hapo ingekuwepo nchi nyingine kura zingeweza kwenda kwa Senegal yawe mengine
 
Kuna kura za imani na kura za maelekezo.

Amini hivyo mkuu. Kama umeshiriki siasa huna haja ya kukaza fuvu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…