Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Nakutana na watoto wawili wakiwa wanampiga ndege akiwa katika Kona moja ya nyumba,umri wao ni kama miaka mitano Kwa kukadiria.
Mmoja anamwambia mwenzake Yule ndege ni wangu lakini tukimpata tutagawana nyama wewe nusu na Mimi nusu. Mashallah nikajikuta nawaza mbali Sana.
Huwa tukiwa wadogo tunakuwa tuna mapenzi baina yetu,kila mtu humjali mwenzake na huwa hatuna tabia ya uchoyo na ubinafsi,hii ndio asili ya mwanadamu mara baada ya kuzaliwa.
Lakini katika malezi ndio tunaanza kufundishwa kuwa wachoyo,kuwa wabinafsi na kutowajali wengine,hii hutokea ima Kwa kujua au kwakutojua. Mtoto anaanza kufundishwa kuficha midoli yake mara pale watoto wenzake wanapo kuja nyumbani kwao kumtembelea, anaambiwa hiyo baiskeli yako usimpe mtoto mwenzako aendeshe asije kuiharibu.
Haya mambo ya baiskeli nakumbuka enzi hizo tukiwa Lushoto Tanga kwenye Kota za chuo cha ccm Lushoto, wenyeji wenyewe wasambaa walikuwa wanatengeneza baiskeli zao za mbao, Kule Kwa sababu kuna milima basi mnaenda mlimani halafu unajiachia basi unashuka na baiskeli Ile mpaka bondeni na Safar imeishia hapo. Mkuu wa chuo kile miaka hiyo alikuwa anafahamiana na wazungu Fulani basi huwa wakija pale Kota na watoto wao ndio mwenzangu na sie ndio tunapata Mda wa kuendesha baiskeli zao na kuinjoy Sana,hawakuwa wachoyo hata kidogo na tulikuwa tunafurahi Sana wanapo kuja pale Kota.
Bahati mbaya Sana jamii yetu inatufundisha angali tukiwa wadogo kujijali Sisi wenyewe,utasikia kauli kama "ukinunua vitu shule uwe Makini wasije wenzako wakakudokolea" au "hakikisha vitu vyako unakula mwenyewe usimpe mtu yoyote" hizo kauli na mengine mengi ya namna hiyo ndio hutujenga na kuwa watu wachoyo,wabinafsi na tusio wajali wengine ukubwani kwetu.
Leo hii hawa viongozi ambao wanajali matumbo yao na familia zao,hawakuanza Tabia hiyo ghafla Tu Ila ni matokeo ya malezi ambayo wamekuwa nayo na matunda yake ndio tunayaona Leo hii. Hawa wajali wananchi wao ambao ndio walio waweka madarakani Leo hii. Kwasababu Wana Ile roho ya umimi katika nafsi zao,Wana choyo katika kugawana keki ya Taifa na wananchi wenzao Kwa ujumla.
Ni viongozi wachache Sana ambao huenda pamoja na malezi yao huko utotoni lakini walikuja kuishi tofauti na kuwathamini wananchi wote,kwao wao shida za wananchi ni shida zao,njaa za wananchi ni njaa zao,ugumu wa Maisha WA wananchi ni ugumu wao pia. Hawa ndio siku zote wanaumiza vichwa ni Kwa namna gani watatatua shida za watu wao,na Kwa namna gani Maisha ya wananchi wengi yawe na unafuu walau wapate uhakika wa Kula mlo WA siku Bila shida,Kwa namna gani wapate huduma za afya Kwa gharama nafuu na mambo kama hayo.
Hapo ndipo ninapokuja kumkumbuka Mwalimu Julius Nyerere ,alikuwa anaumizwa na shida za wananchi wake na adha mbali mbali ambazo alikuwa anakutana nazo huko mikoani akiwa katika ziara zake,inasemwa pale nyumbani kwake Mikocheni kipindi Fulani walitaka kumalizia kuweka lami kipande cha barabara enzi hizo,akasema "mtawekaje lami hapa wakati wananchi wangu hawana hata uhakika wa Kula Yao itakuwaje"?
Na kuna Ile hutuba yake maarufu alisema,Ikulu kuna biashara gani pale mpaka watu wagombee kuingia pale? Na akaendelea Kwa kusema watu ambao wanaguswa na shida za wananchi Ikulu ni mzigo mkubwa Sana!
Nakubaliana nae kabisa kama unataka kwenda Ikulu na unaguswa na wananchi wako hakika ikulu ni dhamana kubwa Sana kwakuwa kila mwananchi anakutazama wewe na ni dhima kubwa Sana kesho mbele ya Mola wako.
Kuna filamu moja ya kihindi inaonyesha jinsi gani rushwa ilivyotawala na uzembe mkubwa WA viongozi katika kuwatumikia wananchi,starring wa movie hiyo aliomba kuitawala India Kwa siku Mia moja Tu ili afanye mabadiriko,na kweli bwana alivyo chaguliwa kuwa Waziri mkuu wa India alifanya mambo mengi Sana kama alivyofanya mtu kazi Jiwe.
Nami naomba siku mia moja hata kama ndotoni niweke mambo Sawa.
Ni hayo Tu!