Hizi ndio nchi barani Afrika zenye idadi kubwa ya watoto ambao hawapo shuleni (Out Of School Children). Nchi namba 3 itakushangaza!

Hiyo namba 3 wazazi wanakataza watoto wao wasisome shule ila waende madrasat tu kukariri vitu visivyo na manufaa maishani mwao
 
Elimu ya darasani kwasasa ni kujifunza Lugha tu basi mengine unakuja kufundishwa na Jamii.

Acha kusikiliza motivational speakers mkuu.

Hawa madaktari mnaowaona wangefundishwa lugha tu watu wangetibiwa vipi? Manesi? Marubani?
 
Tanzania watoto wadogo wote wako bize na usanii kukata mauno
Huko ndiko kwenye ndoto zao

Ova

Kuna muda natamani madaktari wale wenye pesa na viongozi wa taasisi mbalimbali wale wakubwa wangekuwa wanaonesha maisha yao mitandaoni kama wasanii wanavyofanya.

Watoto wetu wanadanganywa sana na hawa wanaojiita Ma-celebrities.

Kila mtoto wa kiume anataka awe kama Rayvanny na wa kike wanataka wawe kama Hamisa Mobetto.

It's sad and pathetic!
 
Acha kusikiliza motivational speakers mkuu.

Hawa madaktari mnaowaona wangefundishwa lugha tu watu wangetibiwa vipi? Manesi? Marubani?
Manesi waliomaliza kusoma miaka kumi iliyopita hawajapata kazi wewe ukienda kusoma leo nani atakupa kazi ?

au basi nisikuingilie kila mtu na bahati yake πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜
 
Na hao walioko shuleni, wapo "wanaohitimu" pasipo kujua kusoma na kuandika
 
Watubebea vitu kupeleka kwenye magari dah ila inhumane maana ndio taifa la kesho hili Mungu waasaidie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…