Hizi ndio nchi barani Afrika zenye idadi kubwa ya watoto ambao hawapo shuleni (Out Of School Children). Nchi namba 3 itakushangaza!

Hizi ndio nchi barani Afrika zenye idadi kubwa ya watoto ambao hawapo shuleni (Out Of School Children). Nchi namba 3 itakushangaza!

Wakuu,

Hivi karibuni, Shirika la Umoja wa Mataifa UNESCO limetoa ripoti mpya inayoelezea kwa undani idadi ya watoto ambao wanastahili kuwepo shuleni lakini kwa sababu tofauti tofauti hawapo shuleni.

Soma pia: Ukatili unaofanyika kwa watoto wa shule binafsi ya EXPERANCIA (Sengerema)

Kulingana na ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), watoto na vijana milioni 244 wenye umri wa miaka 6 hadi 18 duniani kote bado hawajapata elimu, na takriban shule 14,300 zimefungwa katika nchi 24 za Afrika kufikia Juni 2024 kulingana na Baraza la Wakimbizi la Norway (NRC).

Ripoti hiyo imezitaja nchi kama Burkina Faso, the Democratic Republic of Congo, Cameroon, Chad, Nigeria na Niger kama nchi zinaozoogoza kwa kuwa na watoto wengi wasioenda shule huku umasikini ukitajwa kuwa ni sababu kubwa inayopelekea watoto kukosa kwenda shule.

And yes Tanzania pia ipo.

Kulingana na ripoti ya UNESCO hizi ndio nchi zinazoongoza kwa kuwa na watoto wengi wasioenda shule Afrika:

  • Nigeria – 18.18M
  • Ethiopia – 11.1M
  • Tanzania – 6.42M
  • DR Congo – 6.17M
  • Sudan – 5.6M
  • Niger – 5.5M
  • Uganda – 4.9M
  • Angola – 3.9M
  • Burkina Faso – 3.4M
  • Mali – 3.1M
Source: Business Insider Africa, Unesco

Kwa hiyo hapa Tanzania kuna watoto Milioni 6 hwaendi shule, hawa watoto huwa wanafanya nini huko mitaani kama hawaendi shule? Elimu si bure?
Hiyo namba 3 wazazi wanakataza watoto wao wasisome shule ila waende madrasat tu kukariri vitu visivyo na manufaa maishani mwao
 
Elimu ya darasani kwasasa ni kujifunza Lugha tu basi mengine unakuja kufundishwa na Jamii.

Acha kusikiliza motivational speakers mkuu.

Hawa madaktari mnaowaona wangefundishwa lugha tu watu wangetibiwa vipi? Manesi? Marubani?
 
Tanzania watoto wadogo wote wako bize na usanii kukata mauno
Huko ndiko kwenye ndoto zao

Ova

Kuna muda natamani madaktari wale wenye pesa na viongozi wa taasisi mbalimbali wale wakubwa wangekuwa wanaonesha maisha yao mitandaoni kama wasanii wanavyofanya.

Watoto wetu wanadanganywa sana na hawa wanaojiita Ma-celebrities.

Kila mtoto wa kiume anataka awe kama Rayvanny na wa kike wanataka wawe kama Hamisa Mobetto.

It's sad and pathetic!
 
Acha kusikiliza motivational speakers mkuu.

Hawa madaktari mnaowaona wangefundishwa lugha tu watu wangetibiwa vipi? Manesi? Marubani?
Manesi waliomaliza kusoma miaka kumi iliyopita hawajapata kazi wewe ukienda kusoma leo nani atakupa kazi ?

au basi nisikuingilie kila mtu na bahati yake 😂😂😁
 
Dsm pekee ukienda kwenye Makutano ya Barabara Idadi ya Watoto Omba Omba, Waosha Vioo, Mateja nk ni kubwa Mnoo.

Ukizunguka kwenye fukwe za Bahari ya Hindi tokea Mbweni Mpaka Kigamboni wamejaa. Soko la Samaki Ferry na Masoko ya Kkoo wamejaaa watoto ambao kwa kawaida wanatakiwa wawe shuleni lkn cha qjabu Viongozi wanapita na kuangalia pasipo kuchukua hatua.
Watubebea vitu kupeleka kwenye magari dah ila inhumane maana ndio taifa la kesho hili Mungu waasaidie
 
Back
Top Bottom