Hizi ndio Sifa ambazo viongozi wakuu wa nchi huzizingatia wakati wa kuteua viongozi

Hizi ndio Sifa ambazo viongozi wakuu wa nchi huzizingatia wakati wa kuteua viongozi

EllySkyWilly

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2020
Posts
2,204
Reaction score
2,085
Habarini za Leo ndugu na marafiki

Leo nimekuja na sifa ambazo viongozi wakuu huzizingatia wakati wa kuteua wasaidizi wao.

Mfano Rais anapochaguliwa tu, moja ya jukumu lake huwa ni kuteua viongozi watakao simama naye katika kutekeleza majukumu yaliyo mbele yake.

Hivyo ndani ya akili ya Rais hutawaliwa na mawazo mengi tu, Rais huwaza ni nani ataweza kuwa Waziri mkuu, ni nani ataweza kuwa waziri wa wizara ya fedha, ni nani ataweza kusimama kama Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG), nani ataweza kuwa jaji mkuu wa serikali, nani ataweza kuwa waziri wa nishati, nani ataweza kuwa mkurugenzi wa TRA, EWURA, ni nani ataweza kuwa mwanasheria mkuu wa serikali akaweza kuitetea nchi, ni nani ataweza kuwa barozi, ni nani ataweza kuwa mkemia mkuu wa serikali, ni nani ataweza kuwa mkuu wa chuo cha SUA, ni nani ataweza kuwa mkuu wa mkoa fulani n. k.

Viongozi wakuu wote duniani tangu enzi na enzi hutumia sifa zifuatazo wanapo fanya maamuzi ya kuteua wasaidizi wao. Sifa hizi zipo ndani ya kitabu cha Danieli sura ya kwanza ukisoma kuanzia mstari wa kwanza na kuendelea utaziona sifa ambazo mfalme Nebukadneza alizitumia ili kuwapata vijana watakao simama naye kwenye jumba la kifalme yaani ikulu.

Naomba tusome kuanzia mstari wa tatu mpaka 7.

"Danieli 1:3-7
3 Kisha Mfalme Nebukadneza akamwagiza Ashpenazi ofisa mkuu wa makao yake ya kifalme awalete baadhi ya Waisraeli, na kuwaleta ndani wale wanaotoka katika uzao wa kifalme na wa watu mashuhuri.

4. Walipaswa kuwa vijana wasio na kasoro, wazuri wa uso, wajuzi wa hekima, werevu kwa sababu ya maarifa yao, wenye kufahamu elimu, watakaoweza kusimama katika jumba la mfalme; tena alimwambia awafundishe elimu ya Wakaldayo, na lugha yao.

5. Pia, mfalme aliagiza wapewe kila siku vyakula bora ambavyo yeye mwenyewe alikula na divai ambayo alikunywa. Walipaswa kuzoezwa kwa miaka mitatu, na baada ya muda huo wangeanza kumtumikia mfalme.

6. Sasa baadhi ya vijana hao walikuwa wa kabila la Yuda: Danieli, Hanania, Mishaeli, na Azaria.

7. Na ofisa mkuu wa makao ya mfalme akawapa majina; alimpa Danieli jina Belteshaza, akampa Hanania jina Shadraki, akampa Mishaeli jina Meshaki, na kumpa Azaria jina Abednego.

Ukisoma kwa umakini na kutafakari kwa kina katika kitabu hicho unapata sifa zifuatazo.

1. Vijana wawe wa uzao wa kifalme na wa watu mashuhuri. Hapa mfalme aliamini akiwapata baadhi ya vijana wanao tokea katika familia za uzao wa kifalme yaani uongozi na watu mashuhuri basi ni wazi kabisa kwamba watakua na karama na vipawa vya kiungozi na ujuzi ama uzoefu katika kuongoza.

2. Vijana wasio na kasoro. Hapa unatambua wazi kabisa kwamba ni kwanini viongozi hawawezi kuteua watu wenye kasoro. Kasoro inayo zungumziwa hapa ni kasoro ambayo itaathiri kwa namna moja ama nyingine utendaji wake wa kazi. Mfano wa kasoro hizo ni ulevi, makosa ya jinai, kutokuwa na hekima na busara, kuwa na tabia mbaya za kutoa lugha chafu bila kuogopa, uongo, matusi, kutoa rushwa, kutumia nafasi ya uongozi kunyanyasa wanawake kingono, kuchanganya mapenzi na kazi.

3. Wazuri wa uso, hapa wanazungumziwa watu wenye mwonekano wa kuvutia. Hili liko wazi ndugu zangu kuna baadhi ya nafasi za kazi ambazo huhitaji kuweka watu wenye sura nzuri za kuvutia. Hivyo basi watu waliojaliwa sura nzuri za kuvutia pamoja na baadhi ya sifa nilizozitaja hapa huwa na nafasi kubwa sana ya kuteuliwa. Na kwenye makampuni pia wakati wa kuajili huangalia sana sifa hii ya uzuri wa sura na mvuto. Unataka kumwaajiri afisa masoko kwaajili ya kushawishi wateja huwezi kuajili mtu mwenye sura ambayo haina mvuto. Kwasababu wateja wengi cha kwanza huvutiwa na sura kwasababu hiyo afisa masoko mwenye mvuto atakuwa na nguvu kubwa ya kushawishi wateja kuliko mwenye sura ambayo haina mvuto.

4. Werevu kwa sababu ya maarifa yao, katika sifa hii mtu mwerevu kwasababu ya maarifa yake, hapa anazungumziwa mtu mwenye hekima.

6. Wenye kufahamu elimu, hapa wanazungumziwa wasomi mbalimbali katika levo mbalimbali za kielimu. Mfano waziri wa fedha anatakiwa kuwa na elimu ya mambo ya uchumi na fedha n. k. CAG anatakiwa kuwa na elimu ya mambo ya uhasibu. Sasa mtu mwenye elimu ambayo inaendana na nafasi inayohitajika anakuwa na nafasi kubwa mno ya kuteuliwa. Lakini pia ukiangalia waziri wa nishati amewekwa pale kwasababu ana maarifa na mambo ya nishati kwasababu ndio mambo aliyosomea.

7. Wenye uwezo wa kufundishika kwasababu walipaswa wafundishe elimu ya Wakaldayo, na lugha yao. Lakini pia mtu anapo teuliwa kutakiwa kufundishwa majukumu mapya ya kazi yake hiyo mpya. Na wengi wao huwa ni wageni kabisa na mangira hayo ya kazi. Mfano kiongozi mkuu anapo mteua mhadhiri Kutokea chuo kikuu na kumpatia kazi nyingine serikalini swala la kumpata mtu ambaye ataweza kujifunza mazingira ya kazi mpya kwa haraka huzingatiwa sana. Ndio sababu huwa tunaona katika wahadhiri wengi huteuliwa mmoja ambaye yupo smart na ambaye ataweza kujifunza mazingira ya kazi yake mpya kwa haraka kabisa.

Katika sifa zote saba (7) nilizoweza kuzielezea. Sifa moja muhimu zaidi kuliko zote ambayo viongozi wakuu huingalia ni hekima. Ukiweza kuwa na hekima utakubalika kila mahali na kila mtu

Sasa hekima ni nini na inafanyaje kazi katika siasa. Nitakwenda kuelezea nini maana ya hekima na aina za hekima na inafanyaje kazi katika siasa. Soma kwa umakini upate kuelewa itakusaidia sana katika safari yako ya uongozi wa kisiasa. Hata wale mlio teuliwa tayari tafadhari fuatana na mimi ili upate kuelewa jinsi kupita salama katika safari yako ya uongozi.

Maana ya Hekima
Ziko aina nne za hekima:-
Kuna Hekima ya kidunia,
Hekima Tabia ya Kibinadamu, Hekima ya kishetani na
Hekima ya KiMungu au
Hekima ishukayo kutoka juu.

1. Hekima ya kidunia
Hii ni ufahamu unaotokana na kusoma kwingi katika elimu mbalimbali za dunia.
Ukisoma katika hivi vitabu utaweza kuelewa vizuri. (1 WAKORINTHO 2:6), (MATENDO 7:22);

2. Hekima ya Tabia ya Kibinadamu
Huu ni uwezo wa kisiasa ulio kwa wanadamu fulani ambao unawawezesha kuitawala dunia hii au kukubalika kiuongozi katika jamii (YAKOBO 3:1-5) na (1 WAKORINTHO 2:6).
Hii huwa ni tabia tu ya mtu, wakati mwingine tangu utotoni;

3. Hekima ya Kishetani
Ni uwezo wa ziada wa kishetani unaomuwezesha mtu kufanya dhambi kwa ubingwa; (YAKOBO 3:15).

4. Hekima ya Mungu au Hekima Ishukayo Kutoka juu (YAKOBO 3:15; 1 WAKORINTHO 2:6-8).

(i). Ni uwezo wa Ki-Mungu unaokuwa juu ya mtu unaomuwezesha kufahamu njia ya ki-Mungu ya kupata ufumbuzi wa tatizo;

(ii) Ni uwezo wa Ki-Mungu wa kuwaelewesha watu mpaka wanaamua kuyafuata yaliyo ya Mungu kwa furaha na amani.

(iii) Ufahamu usio wa kawaida juu ya mambo ya Ufalme wa Mungu, unaokuwa juu ya mtu (2 PETRO 3:15-16).

(iv) Ufahamu usio wa kawaida unaokuwa juu ya mtu unaomuwezesha kufahamu machache yatakayotokea siku za mbeleni na kufanya maandalizi mazuri kabla hayajatokea (1 WAKORINTHO 12:8).

Hii ndiyo hekima aliyokuwa nayo Yesu na Sulemani, ambayo kila mtu anapaswa kuitafuta kwa bidii.

Thamani ya Hekima ya Mungu
1 Mtu akiwa na hekima ya Mungu atafanikiwa sana katika kazi ambayo imo katika njia ya Mungu (MHUBIRI 10:10).

2 Mtu mwenye hekima ya Mungu ana nguvu (MITHALI 24:5). Maneno ya kinywa chake mwenye hekima yana neema.
Hekima ni ya thamani kuliko lolote jingine (MITHALI 8:11; MHUBIRI 7:11-12; MHUBIRI 9:18; MITHALI 16:16).

Kazi ya Hekima.
1. Kujua jinsi ya kuondoa manung'uniko au mizozo katika jamii (MATENDO 6:1-3);

2.Kujua jinsi ya kukata mashauri au kutoa hukumu (1 WAFALME 3:16-28);

3.Kufahamu yanayotupasa kusema katika majadiliano na mtu wa aina yoyote (MATENDO 6:9-10; LUKA 21:14-15; MATENDO 7:9-10:

4.Kujua jinsi ya kufasuri maneno tunayoambiwa au tunayoyasikia (MHUBIRI 8:1);

5.Kujua wakati wa kufaa wa kuzungumza au kufanya jambo au wakati wa kuonya (MITHALI 25:11-12);

6.Kujua jinsi ya kujibu maswali ya mafumbo na kugundua mafumbo ya kijanja na kibanadamu (2 NYAKATI 9:1-3, 5-7; 2 SAMWELI 14:1-8, 18-19);

7.Kujua jinsi ya kuituliza hasira ya mtu (MITHALI 16:14);

8.Kumwezesha mtu kutamka maarifa (MITHALI 15:2)

9.Hekima itakufundisha ni wakati upi wa kunyamaza au kusema (MARKO 14:55-62).

10.Hekima itakufundisha ni wakati upi wa kukemea (LUKA 13:31-32).

11.Hekima itakufundisha ni wakati upi wa kufundisha kwa kitendo (MARKO 7:1-8) au ni wakati upi wa kujibu swali kwa swali (MATHAYO 21:23-27).

Jinsi ya kupata hekima ya Mungu ili uweze kufanikiwa katika uwanja wa siasa.

1. Ufahamu thamani ya hekima na kutoidharau (MITHALI 14:6);

2.Kuwa mkamilifu au mtakatifu (1 WAKORINTHO 2:6; YAKOBO 3:16-17);

3.Kukubali kuwa mpumbavu (1 WAKORINTHO 3:18);

4.Kuwa mnyenyekevu yaani kuwa mbali na kiburi na majivuno (MITHALI 11:2);

5.Kuwa mwepesi wa kushaurika na kufundishika (MITHALI 19:20);

6.Kumcha au kumhofu Mungu (ZABURI 111:10);

7.Kuenenda pamoja na wenye hekima (MITHALI 13:20);

Hivyo ndugu na marafiki sifa hii kuu ambayo ni hekima viongozi wakuu huitazama sana wakati wa kuteua. Na ndio sababu watu wenye hekima ya Mungu huwa na nafasi kubwa mno kuteuliwa kushika nyazifa mbalimbali kwasababu kwanza kabisa watu hao huwa ni waaminifu, wasikivu, wepesi kushaurika, na kufundishika kuliko wasio na hekima ya kiMungu.

Imeandaliwa na mimi mwenyewe
Ellyskywilly,
Kijana mzalendo,
Mawasiliano ukihitaji ushauri zaidi
ellywilly728@gmail.com.
Mungu ibariki Tanzania
 
Hivi vigezo vinafaa kwenye theocracy. Tanzania ni Republican Democracy. Vigezo vya kikatiba ni vipi?
 
Naimani hata Magufuli anazingatia sifa hizi kuteua wasaidizi wake
Angekuwa anazingatia sifa hizo kazi yake miaka yote 5 isingekuwa teua, tengua, teua, tengua ad infinitum kuliko watangulizi wake wote ikiwa na maana anateua kwa kubahatisha halafu anatengua kujaribu tena. Anateua, anatengua, anateua tena huyohuyo anatengua ili amteue tena! Hapa kazi tu?
 
Ndiyo umetuandikia nini sasa hapa? Kwani ungefanya tu 'Summary' ya haya Maelezo yako marefu na yenye Kuchosa Kuyasoma usingeeleweka pia?
 
Angekuwa anazingatia sifa hizo kazi yake miaka yote 5 isingekuwa teua, tengua, teua, tengua ad infinitum kuliko watangulizi wake wote ikiwa na maana anateua kwa kubahatisha halafu anatengua kujaribu tena. Anateua, anatengua, anateua tena huyohuyo anatengua ili amteue tena! Hapa kazi tu?
Mkuu kuna watu huwa wanabadirika wengine hurubuniwa pia mpaka wanajikuta performance inapungua.
 
Back
Top Bottom