Ukweli mchungu/ukweli ambao wanasimba hawataki kabisa kuusikia masikioni mwao ni ukweli ambao ukiuzungumza utapigwa mawe, matusi na kejeri za hapa na pale.
Kwa hali waliyo nayo wanasimba/mashabiki wasimba haina tofauti na mgonjwa aliyetibiwa kwa muda mrefu bila kutambua kuwa ugonjwa wake atapona lini?? Sasa imebaki faraja na kelele za kisiasa za mpira Kama "baleke ni bonge la chezaji"
"Chama ni fundi kweli kweli"'
Kiufupi mashabiki wa Simba wamejisahau kabisa kuwa hawana uwezo wa kuchukua kombe la Nbcpl, hawana uwezo wakuchukua kombe la CAF, japokuwa wanaimba nakujisifu, kombe la Fa nalo linaupinzani mkubwa hata kombe ngao ya jamii lipo kwa wahasimu wao yanga.
Tumaini kubwa la mashabiki wa Simba/viongozi kwa hivi Sasa ni kumfunga mtani(yanga).
Kidogo hiyo itawafariji lakini yanga asipofungwa, Simba akapigwa basi kocha wa Simba Robertinho atafungasha mzigo wake.
Na, endapo yanga akaifunga Simba, na wydad akapiga kwenye mshono Robertinho ndiyo mwisho wa kibarua chake,
Hizo ndiyo furaha/kombe la mashabiki wa Simba lililobaki ni kushinda nyumbani.
NB: matusi, povu ruksa na tukutane tar 16/4 kwa mkapa uje kushuhudia namna gani yanga akisababisha kocha(Robertinho) akifukuzwa na mikoba kupewa Al watani juma mgunda.