Hizi ndizo drone zilizomfukuzisha Lugola na Andengenye? Basi waombwe msamaha

Hizi ndizo drone zilizomfukuzisha Lugola na Andengenye? Basi waombwe msamaha

CHIZI VITABU

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2021
Posts
1,061
Reaction score
2,477
Kama ndizo drones hizi walizotaka walete wale jamaa wakasiribwa kwelikweli basi waomnbwe msamaha haraka sana maana(siwatetei kwenye ufisadi wao ila kwa hili it was a good idea) kuna siku Kariakoo ile au magorofa marefu yatawaka moto huu mji utaungua wote maana shughuli ya juzi kariakoo imeonyesha dhahiri kwamba hata makao makuu ya fire hayana maji yaani hata visima hawana

Yaani yale mazoezi sijui ya kustukiza airport halafu wanahojiwa kwenye makamera wanajisifu kwamba wako vizuri unaweza kudhani ni watu walio serious kumbe FIX tu ni aibu sana kwa kweli bora hata waliokuwa wanajijibia KWANI SERIKALI NDO IMELETA*&*&(msituambie tena story za maji hayo magari ni mapambo tu siku nyingine ikitokea nyie jibuni kwani SERIKALI NDIYO IMELETA MOTO?

No wonder hata kuzima mlima kilimanjaro ilibidi kwenda kupiga magoti kenya kuomba helicopter, yaani haya ma sky scrappers ya mji huu kuna siku tutatia aibu ya dunia toka enzi za MV Bukoba, matetemeko Kagera, nzige, moto Kilimanjaro, kivuko ukerewe hii nchi imekuwa exposed kwamba haipo tayari kukabiliana na natural disasters UONGOUONGO TU na kutumia mahela mengi kwenye sisasa za uongouongo za kina covid 19 wabunge feki.

HAHAHAHAHAHA JIJI KUBWA LA NCHI YA UCHUMI WA KATI HALINA FIRE HYDRANT HATA MOJA, lol kuna siku hata ofisi nyeti zitaungua moto watu wanaangaliana na kuja na matamko ya kinafiki tu.

 
Kumuomba radhi Lugola naona ujinga tu, yule aliyekuwa anamsifu Magufuli kama Mungu wake hana lolote la maana, yeye Lugola ndie anatakiwa akatubu.
 
Ungetutajia na bei zake ili tuoanishe na bei iliyokuwa imetangazwa na kina Lugola
 
Unaamini wangeleta hizo? Bei waliyoquote unaikumbuka au unaenjoy teknolojia tu
Kama alikuwa na mpango wa kuleta dreamliner jingine kuna ubaya gani ange invest hiyo hela kwenye mambo ya maana ili kuwa able kupambana na natural disasters ndiyo maana nimesema it was a good idea kama bei ya huko Romania ilikuwa ya kifisadi wangecheki alternatives hata kwa Wachina.

Kama inashindikana basi wachukue hata magari ya kisasa ya FAYA NA KUJENGA HYDRANTS FOR GOD SAKE. Kuna nchi zime purify maji ya bahari yanatumika shughuli nyingine jengeni hata reservoir ndogo pembeni ya bahari mpurify kwa ajili ya majanga ya moto, Godamn it
Hela za kuchezea kwa ma DC, makada na wabunge feki kina mdee zipo tu ,kwenye issue za maana ni unafiki n autoto utoto tu.
 
Alikuwa anaongoza jeshi la polisi halafu anakata mauno huku anawakumbatia hao polisi wa kike, he was an embarrassment to the appointing authority.
 
Andiko la kudhani zaidi kuliko kiuchunguzi
Tukio la kariakoo limetia aibu sana hivi magari yao yana hata winchi kweli?gorofa la bandari likiuungua juu kule wanaweza zima au itaundwa tume kuchunguza hujuma?
 
Umeona clip ya moto jana wa nbc kasulu? Kagorofa kamoja tu jamaa wanazima kwa tabu kweli kasimama mtu chini anayoosha mikono na ka horse pipe kama vile ananyeshea bustani nyumbani, soon hii nchi itatia aibu na haya magorofa yanayochipuka kwa kasi.
Nimeona clip moja inamuonesha askari wa zimamoto ameshika mpira maji yameisha akaamua kuanza kupuliza moto kwa mdomo, ndiko tunakoenda, uchumi wa kati huu wa serikali ya viwonder
 
Nimeona clip moja inamuonesha askari wa zimamoto ameshika mpira maji yameisha akaamua kuanza kupuliza moto kwa mdomo, ndiko tunakoenda, uchumi wa kati huu wa serikali ya viwonder
Hahahahaa hela za kina polepole kusajili kina covid 19 zipo kwenye issues za maafa hata visima vya maji ni zero
 
Tukio la kariakoo limetia aibu sana hivi magari yao yana hata winchi kweli?gorofa la bandari likiuungua juu kule wanaweza zima au itaundwa tume kuchunguza hujuma?
sawa na waziri mkuu juzi nimemsikia anasema eti watafanya tathmini kuona ni hasara kiasi gani imepatitikana, sijui ili wafanyaje wakishajua ??, maana sijawahi kuona serikali hii inawalipa watu fidia ya hasara walizopata, kwa hiyo lile tamko la waziri mkuu majaliwa lilikuwa porojo tu, naamini ndio kimya na hatakuja kuongea lolote, kwani hata baada ya kutoa tamko la kusimamisha shughuli pale sokoni kariakoo juzi, (bila kutaja muda), siku iliyofuata yaani jana nikasikia mkuu wa mkoa makalla anasema wafanyabiashara wanatakiwa warudi kuendelea na shughuli zao hapo sokoni
 
issiue sio drones, issue ambulance itachukua muda gani kufika eneo la tukio?
 
Back
Top Bottom