Hizi ndizo sababu za CHADEMA kuanzia mikutano yake Mwanza

Hizi ndizo sababu za CHADEMA kuanzia mikutano yake Mwanza

voicer

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2020
Posts
5,545
Reaction score
11,944
Mwanza ni karibu na Mikoa ya Geita, Mara, Kagera, Kigoma, Simiyu, Tabora na Shinyanga kijiografia.

Ni Rahisi kusafirisha wafuasi kiduchu, kutoka mikoa hiyo na wilaya zake na hatimae kuwajaza Mwanza. Pia Mwanza Chadema inawategemea wafuasi wa Ezekiah Wenje,ambao kwa ujumla hawafuati sera bali ukabila wao.

Ni kawaida ya hiyo jamii,mifano halisi ni kule kenya kwa "Baba" yao Raila.

Na kule Mwanza jamii hiyo imejikita kwa wingi na Chadema inatarajia kunufaika nao kwa asilimia kubwa!

Tofauti na Mikoa kama Dar es Salaam au Arusha, ambako hata Chadema yenyewe haina uhakika na kiwango kilichosalia cha ushawishi wake huko. Baada ya kuwa na mabadiliko makubwa ndani ya miaka sita ambayo CCM wameitumia kujijenga huko.

Kwa kutekeleza ilani na ahadi zao kama inavyoendelea mpaka sasa. Kwa Msaada wa Zakaria na Mabasi yake!

Ni rahisi John Heche na Chadema kuwasafirisha wafuasi wake ambao wana Chuki na CCM, baada ya kudhibitiwa biashara za Magendo ya mipakani sanjari na wale wa Tunduma. Na kuwapeleka Mwanza kwa urahisi na kujaza viwanja vya Furahisha kisha wakasema Mwanza wameipokea Chadema kwa wingi,kumbe changa la macho.

Pia! Gharama na miundombinu ya usafiri, kanda ya ziwa ni Rahisi sana kuwasafirisha kwa uchache wao.
Na kuwakutanisha Mwanza kwa malori, Coaster na nyenzo zozote zile za usafirishaji. Chadema pia bado wana ndoto za kutumia kifo cha Alphonce Mawazo wa Geita,na kutumaini kupata wafuasi kutoka Geita pale watakapolitumia jina lake Majukwaani.

Chadema Moshi na Arusha, hata kwa Mbowe mwenyekiti kule Hai, tathmini yake inaonyesha kuchokwa!
Watu wameona tofauti kubwa, kwa vipindi viwili tofauti. Enzi ya siasa za Uhuni wa Lema na Arusha, wakifikia hata kuhamasisha wafuasi wao, kutosalimiana na kuzira misiba ya wapinzani wao CCM.

Na Enzi za Maendeleo na siasa za kistaarabu,baada ya Lema kupigwa chini. Ambapo Arusha imerudisha hadhi yake na miradi ya Maendeleo inavyotekelezwa kwa kuibadili Arusha mpaka sasa. Pia Hai mambo yalibadilika na siasa pia zikabadilika!

Lakini kinachowanyima Uhakika Chadema mpaka sasa. Hawajui ni nini wananchi wanacho vichwani mwao, pale wanapooona Sabaya akifanyiwa uhuni na genge la Mbowe mpaka sasa.

Mbeya Tulia Akson, ameikamata Mbeya na wameona tofauti baina ya vipindi viwili tofauti pia. Enzi ya Siasa za kihuni za Sugu jijini Mbeya ambapo ilikuwa kufukuzana na FFU kila uchao. Mbeya ikawa ikinuka moshi wa mabomu ya Machozi.

Lakini sasa Mbeya chini ya Tulia Akson ambapo Mbeya imetulia na inasonga mbele kimaendeleo, katika nyanja zote na wananchi wameona utofauti huo, Hivyo Mwanza imekuwa Chaguo sahihi, kwa Chadema kuanzia kupima upepo.

Lakini sababu kubwa ikiwa ni urahisi wa miundombinu ya kusomba wafuasi toka mikoa tofauti ambayo imepakana na Mwanza ili kuuhadaa Ulimwengu kwamba Bado wako na uungwaji mkono,lakini ukweli ni tofauti na Uhalisia.

Nimetupa jiwe hilo, kama kawaida litakayempata gizani au kwenye mwanga. Kwa utamaduni wa Chadema! Matusi ni jibu sahihi kwa liliempata vizuri.

Alamsikhi.

10101.
 
We jamaa kumbe huwa uko weak namna hii!

Au umeamua tu kujitoa akili kwa maslahi ya chama chako?

Muhimu kwako linda heshima yako.
Mkuu denooJ!

Tunaandika yote tunayopata nafasi ya kuyajua.

Heshima yangu hailetwi na kuitetea Chadema!

Heshima yangu itakuwepo pale nitskaposimamia ukweli.

Heshima ya kweli,inaletwa na Matendo ya kweli,na sio ya unafiki au uongo uongo.

Mimi huwa sitetei Chama, bali nasimamia ukweli,ndio maana hata Post zangu huwa sio za ki-kada!
Bali ni za kuusema ukweli uliopo!

No matter, ni upande gani.
 
Mkuu denooJ!
Tunaandika yote tunayopata nafasi ya kuyajua...
Nimefurahi ulipokiri heshima yako inaletwa na matendo ya kweli, bahati mbaya wewe umeandika uongo mwingi sana hapa.

Mfano, uliposema Chadema inawategemea wafuasi wa Wenje Mwanza [paragraph yako ya pili] huu ni uongo wako kwanza.

Wenje alilelewa na Chadema, wafuasi aliwapatia Chadema, ndio maana alipogombea ubunge kupitia Chadema aliwahi kushinda..

Baada ya hapo Wenje akapoteza, Chadema ikapeleka mgombea mwingine jimbo la Nyamagana 2020, yule dogo licha ya ugeni wake kisiasa [jina nimesahau kidogo] naweza sema alikuwa mshindi wa lile jimbo..

Kama isingekuwa zile hila zenu za uchaguzi 2020, na endapo Wenje alikuwa "star" kama ulivyodai, basi naamini angeondoka na wafuasi wake Nyamagana, lakini haikuwa hivyo.

Having said that, inaonesha kwamba, Chadema haiwezi kumtegemea mtu binafsi kwa manufaa yao, ile taasisi imejengwa in such a way kwamba, anayepewa nafasi ya kugombea kupitia kile chama lazima aaminiwe na wananchi.

Naweza kutoka nje ya hapo, nikakupa mfano mwingine kuonesha vile Chadema haiwezi, na haijawahi kumtegemea individual.

2015 Lowassa akiwa na kashfa ya ufisadi, na kila mtu akimuona hivyo, alihamia Chadema, alipofika kule mafuriko aliyopata kama mgombea wa Chadema mpaka leo yameweka rekodi, na idadi ya kura alizopata milion 6 mpaka leo ni rekodi kwa wapinzani.

Hii inaonesha Chadema inaaminiwa kwa kiasi kikubwa na watanzania, na haiwezi kumtegemea mtu binafsi, tofauti na ulichoandika.

Pia, kuondoka kwa kina Dr. Slaa, Zitto na wengine bado ni mifano zaidi kuonesha nguvu ya Chadema kama taasisi, kwani licha ya kuondoka hao jamaa, bado nguvu ya Chadema imeendelea kuthibitika nchini.
 
Uzuri jf wengi wana uelewa mzuri. Utaishia kudharaulika tu
Sitafuti kupendwa hapa JF!

Sipo humu kuandika ili niheshimike!

Ingekuwa natafuta heshima,ningeweka Identity yangu!

Au namba ya simu kama wafanyavyo wasaka heshima na uteuzi.

Mimi ni voicer of the Voiceless!

No matter ni upande gani....

Iwe CCM au Chadema au upinzani popote..

Mimi huwa naweka Rula juu ya karatasi.
 
Nimefurahi ulipokiri heshima yako inaletwa na kutetea ukweli, bahati mbaya wewe umeandika uongo mwingi sana hapa...
Huyo mtu aliyegombea kwa tiketi ya CHADEMA wewe mwenyewe humjui anaweza kuwa na ushawishi wa kumshinda Mabula?
 
Nimefurahi ulipokiri heshima yako inaletwa na kutetea ukweli, bahati mbaya wewe umeandika uongo mwingi sana hapa...

Mfano, uliposema Chadema inawategemea wafuasi wa Wenje Mwanza [paragraph yako ya pili] huu ni uongo wako kwanza...
Rudia kasome vizuri

Sijasema Chadema inamtegemea Wenje!

Nimesema Chadema inawategemea wafuasi wa Wenje,kwa pale MwanzaCity na pia kutokea Rorya,ambako siasa zao hazitegemei hoja,bali zimekaa kwa Ujaluo wao zaidi.

Nikatolea mfano wa wajaluo wa Luo Nyanza kule Kisumu,Makindu Bay na Homa Bay wanavyomuabuda Raila "Baba"

Kuhusu kuondoka kwa Dk Slaa na waandamizi wengi ndani ya Chadema!

Huwezi kuona madhara yake,sababu wewe unachoangalia nibkuwepo kwa chama tu.

Ila hauangalii kiwango cha Performance yenu.

Na hujiul8zi kwamba kama chama, mngekuwa hatua gani kama hao wote walioondoka wangekuwepo ndani ya chama mpaka tunavyoongea na kuandika humu?

Chama ni taasisi kubwa,haiwezi kufa kifo kama cha binadamu,tutakiacha kikiwepo,ila suala ni kikiwa katika hali gani?

20230113_080002.jpg
 
Rudia kasome vizuri......

Sijasema Chadema inamtegemea Wenje!
Nimesema Chadema inawategemea wafuasi wa Wenje,kwa pale MwanzaCity na pia kutokea Rorya,ambako siasa zao hazitegemei hoja,bali zimekaa kwa Ujaluo wao zaidi...
Wewe ndie hunisomi vizuri, rudia kunisoma, nimeandika vizuri na bahati nzuri umeni quote.

Ndio maana nimekwambia, kama Chadema ingekuwa inawategemea wafuasi wa Wenje, basi Wenje angeondoka na wafuasi wake na kusababisha nguvu ya Chadema kupungua/kwisha Nyamagana, lakini uhalisia hauko hivyo.

Kuhusu kuondoka kwa kina Slaa, napo kama kungekuwa na madhara unayosema basi yangeonekana tu, kwanini yajifiche? kutokuyaona maana yake hayapo, usiishi kwa hisia.

Hiyo picha uliyoweka nayo haina maana yoyote kuonesha chama hakina nguvu ya watu, hilo ni jengo tu, lililojengwa na wale waliopo sehemu husika kwa matumizi yao kwa wakati husika, haiwezekani watanzania wakaichangia Chadema kujenga ofisi zao nchi nzima mpaja vijijini.
 
Sitafuti kupendwa hapa JF!

Sipo humu kuandika ili niheshimike!

Ingekuwa natafuta heshima,ningeweka Identity yangu!

Au namba ya simu kama wafanyavyo wasaka heshima na uteuzi.

Mimi ni voicer of the Voiceless!

No matter ni upande gani....

Iwe CCM au Chadema au upinzani popote..

Mimi huwa naweka Rula juu ya karatasi.
Kuna raia hapo Geita kakamatwa na kuwekwa mahabusi kisa Anadai haki yake ya kikatiba ya kupatiwa maji Safi na salama,middle class umefwata mkia wako, huwezi kuanzisha mada bila ya kuwahusisha CDM
 
Huyo mtu aliyegombea kwa tiketi ya CHADEMA wewe mwenyewe humjui anaweza kuwa na ushawishi wa kumshinda Mabula?
Kusahau haliwezi kuwa kosa la jinai, na wala hakuwezi kufuta uhalisia, uhalisia utabaki pale pale..

*Anaitwa Pambalu, yuko na cheo Bavicha.
 
Asante kwa analysis yako, binafsi natamani siasa sawa za ushindani vyama viwe vinapokezana madaraka na sio chama kimoja miaka 60 bila kutatua ata tatizo moja kwa 100% iwe maji, umeme, elimu, afya au miundombinu, chama cha hivyo kinahitaji miaka mingine mingapi kuleta maendeleo ya kweli?
 
Sitafuti kupendwa hapa JF!

Sipo humu kuandika ili niheshimike!

Ingekuwa natafuta heshima,ningeweka Identity yangu!

Au namba ya simu kama wafanyavyo wasaka heshima na uteuzi.

Mimi ni voicer of the Voiceless!

No matter ni upande gani....

Iwe CCM au Chadema au upinzani popote..

Mimi huwa naweka Rula juu ya karatasi.
HOJA Yako Haina mizania.

CDM Haina RUZUKU, ipate wapi pesa kisafirishwa Wanachama Kwa maelfu kama ulivyokiri watajaza mkutano?

Nikisoma btn the lines,

Unaitisha CCM juu ya yatakayojiri Furahisha mza!!!
 
Rudia kasome vizuri......

Sijasema Chadema inamtegemea Wenje!
Nimesema Chadema inawategemea wafuasi wa Wenje,kwa pale MwanzaCity na pia kutokea Rorya,ambako siasa zao hazitegemei hoja,bali zimekaa kwa Ujaluo wao zaidi.

Nikatolea mfano wa wajaluo wa Luo Nyanza kule Kisumu,Makindu Bay na Homa Bay wanavyomuabuda Raila "Baba"

Kuhusu kuondoka kwa Dk Slaa na waandamizi wengi ndani ya Chadema!

Huwezi kuona madhara yake,sababu wewe unachoangalia nibkuwepo kwa chama tu.

Ila hauangalii kiwango cha Performance yenu.

Na hujiul8zi kwamba kama chama...
...mngekuwa hatua gani kama hao wote walioondoka wangekuwepo ndani ya chama mpaka tunavyoongea na kuandika humu?

Chama ni taasisi kubwa,haiwezi kufa kifo kama cha binadamu,tutakiacha kikiwepo,ila suala ni kikiwa katika hali gani?

View attachment 2485559
Kuna thread umeandika msoga gang wawampendi Majaliwa imefutwa,

Nakushauri badili heading lisiwepo neno msoga gang na upost tena.

Heading yaeza kuwa, "Majaliwa hapendwi na wafuatao" maudhui yabaki vile vile.
 
Back
Top Bottom