Mwanza ni karibu na Mikoa ya Geita,Mara,Kagera,Kigoma,
Simiyu,Tabora na Shinyanga kijiografia.
Ni Rahisi kusafirisha wafuasi kiduchu ,kutoka mikoa hiyo na wilaya zake na hatimae kuwajaza Mwanza.
Pia Mwanza Chadema inawategemea wafuasi wa Ezekiah Wenje,ambao kwa ujumla hawafuati sera bali ukabila wao.
Ni kawaida ya hiyo jamii,mifano halisi ni kule kenya kwa "Baba" yao Raila.
Na kule Mwanza jamii hiyo imejikita kwa wingi na Chadema inatarajia kunufaika nao kwa asilimia kubwa!
Tofauti na Mikoa kama Dar es Salaam au Arusha,ambako hata Chadema yenyewe haina uhakika na kiwango kilichosalia cha ushawishi wake huko.
Baada ya kuwa na mabadiliko makubwa ndani ya miaka sita ambayo CCM wameitumia kujijenga huko.
Kwa kutekeleza ilani na ahadi zao kama inavyoendelea mpaka sasa.
Kwa Msaada wa Zakaria na Mabasi yake!
Ni Rahisi John Heche na Chadema,kuwasafirisha wafuasi wake.
Ambao wana Chuki na CCM, baada ya kudhibitiwa biashara za Magendo ya mipakani sanjari na wale wa Tunduma.
Na kuwapeleka Mwanza kwa urahisi na kujaza viwanja vya Furahisha.
Kisha wakasema Mwanza wameipokea Chadema kwa wingi,kumbe changa la macho.
Pia!
Gharama na miundombinu ya usafiri,kanda ya ziwa ni Rahisi sana kuwasafirisha kwa uchache wao.
Na kuwakutanisha Mwanza kwa malori,Coaster na nyenzo zozote zile za usafirishaji.
Chadema pia,bado wana ndoto za kutumia kifo cha Alphonce Mawazo wa Geita,na kutumaini kupata wafuasi kutoka Geita,pale watakapolitumia jina lake Majukwaani.
Chadema Moshi na Arusha,hata kwa Mbowe mwenyekiti kule Hai,tathmini yake inaonyesha kuchokwa!
Watu wameona tofauti kubwa,kwa vipindi viwili tofauti.
Enzi ya siasa za Uhuni wa Lema na Arusha,wakifikia hata kuhamasisha wafuasi wao, kutosalimiana na kuzira misiba ya wapinzani wao CCM.
Na Enzi za Maendeleo na siasa za kistaarabu,baada ya Lema kupigwa chini.
Ambapo Arusha imerudisha hadhi yake na miradi ya Maendeleo inavyotekelezwa kwa kuibadili Arusha mpaka sasa.
Pia Hai...
Mambo yalibadilika na siasa pia zikabadilika!
Lakini kinachowanyima Uhakika Chadema mpaka sasa!
Hawajui ni nini wananchi wanacho vichwani mwao,pale wanapooona Sabaya akifanyiwa uhuni na genge la Mbowe mpaka sasa.
Mbeya!
Tulia Akson,ameikamata Mbeya na wameona tofauti baina ya vipindi viwili tofauti pia.
Enzi ya Siasa za kihuni za Sugu jijini Mbeya,ambapo ilikuwa kufukuzana na FFU kila uchao.
Mbeya ikawa ikinuka moshi wa mabomu ya Machozi.
Lakini sasa Mbeya!
chini ya Tulia Akson,mbapo Mbeya imetulia na inasonga mbele kimaendeleo,katika nyanja zote.
Na wananchi wameona utofauti huo!.
Hivyo Mwanza imekuwa Chaguo sahihi,kwa Chadema kuanzia kupima upepo.
Lakini sababu kubwa ikiwa ni urahisi wa miundombinu ya kusomba wafuasi toka mikoa tofauti ambayo imepakana na Mwanza.
Ili kuuhadaa Ulimwengu kwamba Bado wako na uungwaji mkono,lakini ukweli ni tofauti na Uhalisia.
Nimetupa jiwe hilo......
Kama kawaida....
Litakayempata gizani au kwenye mwanga.....
Kwa utamaduni wa Chadema! Matusi ni jibu sahihi kwa liliempata vizuri......
Alamsikhi.
10101.