Pre GE2025 Hizi ndizo sababu za kwanini Serikali ya CCM haitaki Maandamano ya CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
uko sahihi kabisa umeelezea vizuri hulka yako na wenzie na jinsi haiba zenu na hao ulowaelezea zinalandana na kushabihiana mujarabu sana

January 24 virungu day,
virungu vitakua vikali sana.....

my friend elewa ni virungu vikali sana kwa nyumbu au panyarodi atakaejitokeza kwenye siku ya fujo chadema January 24 🐒
 
Chada hawajawahi kupoteza nguvu kwenye jamii. Ispokuwa jpm alijaribu kutumia vyombo vya Dolla kuzuia nguvu hiyo upepo ukampitia yeye akafa kifo Cha mende
 
Chadema nao wamekosea target. Kuandamana kwa ajili ya mambo ya uchaguzi inaonyesha mnafikiria zaidi nafasi kuliko maisha ya kawaida.

Walitakiwa kuwa na ajenda zingine kama umeme na kupanda kwa gharama za maisha. Mwananchi wa kawaida utampeleka barabarani kwa kila kinachomgusa directly na sio indirectly kama sheria ya uchaguzi
 
Na hii ni kutokana na vyama hivi kunga'ng'ania njia na mbinu za zamani kuendesha nchi.
Vyama vingi vikongwe kusini mwa Sahara vimekuwa vikitumia nguvu kubwa kubaki madarakani badala ya kuleta maendeleo.
Jambo ambalo ni sawa na kujiangamiza mwenyewe. Kwani kadri ugumu wa maisha unavyozidi ndivyo wananchi wanakosa uvumilivu kwa serikali.
Na siku hiyo pia si ajabu mfumo wa interbet ukazimwa.
Right!
 
Hii ya kuandamana kwa mambo yanayomgusa mwananchi ni sahihi kabisa lakini kinachoendelea ni siasa za kutegana.
Yaani CHADEMA wamewatega CCM kwenye mtego ambao CCM wanajua huu ni Mtego ndio maana CHADEMA hawataki kuja direct kama maandamano ya ugumu wa maisha sababu wanajua wakija hivyo nguvu itakayotumika kuzima maandamano hayo ni mara 7 ya hii ya sasa.
Ingawaje naona pia CHADEMA kama watashindwa haya ya mswaada wa sheria za uchaguzi basi waitishe maandamano mengine ya kupinga ugumu wa maisha, umeme ,ufisadi n.k
 
Natabiri mwaka 2025 Wabunge wa Upinzani watakuwa wengi Bungeni.
Hili litawezekana ikiwa tu CHADEMA watakubali kuingia front kwa hali na mali katika kuwa bega kwa bega na jamii ambayo kwa sasa ni kama serikali imewatupa .
 
Hapa kijijini kwetu huwa wanasema waliambiwa na mwenyekiti wa kijiji kwamba CHADEMA imekufa.Sasa wanaogopa maiti?🤣🤣🤣🤣
Utakufq wewe na mwenywkiti wako kama jiwe alivokufa na bahari ikatulia cdm ikizidi kumea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…