Don Gorgon
Member
- Nov 21, 2024
- 35
- 68
Tangu Rais Samia alipopokea kijiti cha uongozi wa nchi mwaka 2021, amesifiwa na baadhi ya Watanzania kama Mama mwenye moyo wa ukarimu, hususan katika kujitoa kwa hali na mali pale anapodhani anaweza kusaidia kwa kutumia fedha ili kuhakikisha mambo fulani yanaenda vizuri. Wanaona kuwa huu ni mfano wa uongozi wa kujali na una manufaa kwa jamii.
Baadhi yao wanasema kuwa, ikiwa Rais angeamua kutumia pesa hizo kwa matumizi binafsi badala ya kugawana na wananchi, hakika angeweza kufanya hivyo bila matatizo yoyote. Wanaamini kuwa ni jambo la kufurahisha kwamba Rais anachagua kugawana rasilimali na wananchi wake.
Hata hivyo, kuna kundi la wananchi linaloamini kwamba ukarimu huu umekuwa mzigo kwa uchumi wa taifa. Wanaona kwamba fedha hizi, ambazo ni matokeo ya jasho la Watanzania, zinatumika kinyume na matarajio, hasa ikizingatiwa kuwa nchi bado inakabiliwa na changamoto za utoaji wa huduma muhimu kwa wananchi wake. Wananchi hawa wanahisi kwamba fedha zinazopaswa kuelekezwa kwenye miradi ya maendeleo ya muda mrefu na yenye manufaa kwa jamii yote zinatumika kwenye shughuli za muda mfupi ambazo zinawanufaisha watu wachache tu.
Hoja zao ni kwamba kwa hali ya sasa ya uchumi, mkono wa ukarimu wa Rais unapaswa kuwa wa tahadhari ili kuepuka kudhoofisha kibubu cha taifa, ambacho bado kinakabiliwa na changamoto nyingi.
Lakini pia wapo wanaodhani huu ni mkakati tu wa kisiasa ili kushawishi wapiga kura. Kwamba taasisi, vikundi tofauti pamoja na watu binafsi wanaopitiwa na mkono mrefu wa Rais wanawekwa kwenye 'kumi na nane' na pia huenda ni mkakati wa kuendelea kubaki miyoni na vinywani mwa wapiga kura kwa chapa ya "Rais mwenye moyo safi."
Wewe mtazamo wako ni upi?
ZAWADI, MISAADA NA MICHANGO ILIYOTOLEWA NA RAIS SAMIA TANGU 2021
- Rais Samia: Serikali imempatia Mzee Mwinyi zawadi ya gari aina ya Benz ya chini
- UVCCM wawili waliotembea kwa miguu kutoka Dar hadi Musoma wapewa zawadi na Rais Samia. Hongera zao Km 1400 sio mchezo
- Rais Samia atoa msaada wa mahitaji kwa watoto njiti Kigoma
- Wizara ya Katiba na Sheria yazindua "Mama Samia Legal Aid Campaign" mkoani Iringa. Nchi yetu inaenda wapi?
- Rais Samia atoa Tsh Bilioni 1 ili Taifa Stars wafuzu Kombe la Dunia
- Tetesi: - Rais Samia atoa ndege kwaajili ya kusafirisha msiba wa Le Mutuz
- Injinia Hersi: Rais Samia atoa ndege kuipeleka Yanga Mbeya
- Rais Samia atoa tsh 5,000,000 kumuenzi Chifu Mkwawa kwenye kumbukumbu ya miaka 120 ya kifo chake!
- Rais Samia atoa Milioni 2 kwa anayekumbatia Watoto hospitali ya Amana
- Kuelekea 2025 - Rais Dkt. Mwinyi achangia milioni 100 ukarabati wa Kanisa Katoliki Zanzibar
- Rais Samia atoa Ndege kuipeleka Taifa Stars Morocco
- Rais Samia aipa Taifa Stars Milioni 700 kufuzu AFCON
- Rais Samia achangia mamillioni ya pesa taasisi ya profesa Jay Foundation, atoa maagizo mazito kwa Wizara ya Afya na Muhimbili
- Rais Samia awapa Coaster mpya shule ya wasichana Lindi, atoa onyo kali kwa watakao litumia kwa sendoff na kitchen party
- Rais Samia atoa zawadi ya Tsh. Milioni 10 kwa Askofu Mollel, aagiza barabara iwekwe lami!
- Rais Samia alimkabidhi Mbowe TSH 150 million za Mchango wa KKKT - Hai. Huku ni Kuaminika Kulikotukuka!
- Kuelekea 2025 - Rais Samia atoa milioni 10 kwa Bodaboda Arusha
- Rais Samia achangia shilingi milioni kumi mfuko wa yatima na wajane mkoa wa Dodoma
- Kuelekea 2025 - Rais Samia achangia shilingi milioni 50, ujenzi wa shule ya Msingi na ujenzi wa majengo ya Zahanati inayomilikiwa na Bakwata Simiyu
- Kuelekea 2025 - TAKUKURU hamuoni hizi Rushwa: Rais Samia achangia milioni 35, Mbunge na Mkuu wa Mkoa Songwe waongeza Milioni 11.5
- Kuelekea 2025 - Rais Samia “amzawadia” Millioni 10 Askofu Ruwa’ichi Kwa kutambua mchango wake kwa Kanisa na Taifa
JANUARY
- Kuelekea 2025 - Rais Samia ampigia simu Kuhani Mussa na kumuahidi mchango wa Tsh. Milioni 100 ujenzi wa kanisa!
- Rais Samia amzawadia TSh Milioni 5 aliyewaokoa Watumishi wa TRA waliovamiwa Tegeta