Hizi ndo sababu 5 kwanini Telegram ni bora mara 100 kuliko WhatsApp

Hizi ndo sababu 5 kwanini Telegram ni bora mara 100 kuliko WhatsApp

Tunatumia WhatsApp kwa sababu ya mazoea tu ya mtaani, lakini kiufundi, Telegram ipo miaka mia mbele. WhatsApp ni kama usafiri wa umma, lakini Telegram ni mnyama mwingine kabisa.

Mambo yako hivi kifupi doti kwa doti: 👇

1. Cloud Storage: Telegram haijazi Memory ya simu yako hata MB moja; kila kitu kinalindwa kwenye seva zao. Ukibadilisha au kupoteza simu leo, unakuta chat na picha za miaka mitano iliyopita zipo palepale bila kuhitaji dharura ya ku-backup.

2. Kutuma Ma-File ya Makubwa: WhatsApp inaleta pozi ukituma faili kubwa na inakata ubora wa picha. Telegram inakubali kutuma file moja la hadi GB 2 bure! Unaweza kutuma movie nzima ya HD au software kubwa bila kupunguza ubora hata nusu.

3. Ulinzi wa Namba yako: Kwenye WhatsApp, ili uchat na mtu lazima amiliki namba yako ya simu. Telegram unaweza kuficha namba yako isionekane na kiumbe yeyote, kisha ukatumia Username tu kuwasiliana mtaani kwa usalama zaidi.

4. Ma-Group ya Jeshi na Bots: Group la Telegram linachukua hadi watu 200,000 kwa pamoja bila simu yako kukwama. Pia lina "Bots" (wasaidizi wa kidijitali) wanaoweza kukutafutia vitabu feki, kukupakulia nyimbo, au kusimamia magroup kimyakimya.

5. Kufanya Kazi Simu Ikiwa Imezima: Telegram ya kwenye kompyuta inajitegemea 100%. Hata kama simu yako kuu imezima chaji, imepotea, au haina internet, bado unaweza kuendelea kuchat na kufanya kazi kwenye PC yako kama kawaida.

Ukweli ni kwamba Mark Zuckerberg anasubiri Telegram wagundue kitu (kama Channels au kuficha meseji) kisha yeye anakinakili na kukileta WhatsApp kwa mbwembwe. Ukishaijua Telegram, kurudi WhatsApp ni kama kurudi nyuma kiteknolojia!
Pamoja na hayo kwa nini haina watumiaji wengi kama WhatsApp?
 
Pamoja na hayo kwa nini haina watumiaji wengi kama WhatsApp?
Telegram sio ndogo Ina mamia ya mamilioni ya watumiaji whatsapp Ina watumiaji billion 2 sababu ni kwamba whatsapp, Facebook na Instagram chini ya meta zilianza mapema kwahiyo kumshawishi mtu kuhama sio rahisi hata hivyo wafanyabiasha na watu wa Teknologia (IT) nk wanatumia telegram kutokana na manufaa niliyoelezea hapo juu.
 
Telegram hana mpinzani kabisa, japokuwa nchi nyingi zimekuwa zinaipiga vita sana. lakini hawajawahi kusema kitu wala kurudi nyuma. alafu walivyowagumu sijawahi kuona hata matangazo yao kama kampuni zingine zinavyojitangaza kwa nguvu 😂😂😂😂
Ukiona hivyo ujue wanapinga pesa ndefu na wanatumia kauli ya " when you win you stay quiety"
 
Nilishawahi kuchakata mbususu ya telegram enzi hizo inaonyesha location. Unaangalia nani Yuko karibu unamsemesha🙂
 
Back
Top Bottom