Hizi ni baadhi tu ya faida za kusoma vitabu

Hizi ni baadhi tu ya faida za kusoma vitabu

Napenda sana kusoma Biography aiseee
Miaka ya nyuma wakati natafuta kutegua kitendawili cha "Kwanini nchi zingine ni tajiri na nchi zingine maskini" na kitendawili cha "Historia ya ulimwengu & MTU MWEUSI".....baada ya pitapita ya huku na huko articles,magazine,forums,documentary,films na books,kitendawili kikafunuliwa mithili ya jigsawpuzzle..Ulivyoandika wapenda biography ukanikumbusha singapore story na benevolent dictator Lee Yuan Kew wake,yeye katika vitabu vyake,interview anasema anapenda kusoma sana autobiograhy na biography.
 
Kitabu kinauwezo wa kukupeleka kwenye ulimwengu wa kale kabisa wa Socrate na Plato
 
Inategemea pia na aina za vitabu mtu asomavyo. Kuna baadhi ya vitabu ni hasara kwa ukuaji wa ubongo
 
Uzi wako ni mzuri sana, ila naamini utapata like yangu tu au chache sana. Kusoma vitabu kwa wengi wetu kunahitaji kufanyika maombi kwanza.
Kwani ameandika ili apate likes nyingi?
 
Jamani lkn kusoma kazi pia! mwee!! labda nisome ''kikosi cha kisasi!.... kikomo! six days war! ubeberu utashindwa,.....one stp forward'' JF udaku, G/forum, Epigate, Quora! MICHUZI....aaaaah!

yaani hapo nitavimaliza dakika sifuri! sili, siogi, silali wataniona mchawi tu uongo bujibuji!

lkn unambia eti nisome KIM IL SUNG na Demokrasia ya juche?? UJamaa by jk nyerere!! au eti kitabu kimeandikwa Mapinduzi Matukufu ya Ayatollah Khamenei? maweee!! utaniua nakwambia!

kwanza naona km unani sinyaisha ubongo!! miayo yake sasa!! saana nitalala hapooo! nikiamka ntaenda kula vihepe tu!
 
FAIDA KUMI (10) ZA KUSOMA VITABU.

1. Ni chakula cha ubongo. Bila kusoma ubongo unadumaa. Hivyo inakupasa kusoma ili kukuza ubongo/akili yako.

2. Vitabu vinakufikisha mahali popote duniani. Utapata kufahamu mazingira na maisha ya watu wengine waishio mbali. Ninaye rafiki, anafahamu miji na mitaa ya Uingereza utadhani ameishi huko. La hasha! Anasoma sana vitabu.

3. Unataka kuwa mzungumzaji mzuri?. Soma sana vitabu. Maana vinakuza stadi ya lugha, ambayo itakusaidia kukuza ulumbi wako. Mlumbi ni mtu mwenye uwezo wa kuzungumza kwenye hadhara.

4. Vitabu ni chanzo cha Hekima. Fanya utafiti, mtu anayesoma sana vitabu huwa na uwezo mkubwa wa kutafakari na kufanya maamuzi sahihi. Maneno na matendo yake ni yenye kujenga na kupendezwa na jamii. Mwenye hekima hazungumzi visivyo na maana, haropoki hovyo, hajivuni. Hushauri mema, huleta suluhisho la migogoro, huleta mawazo chanya katika jamii.

5. Hupunguza msongo wa mawazo. Soma sana vitabu ili kupata utulivu wa fikra. Ondokana na 'stress' kwa kusoma vitabu.

6. Unataka kuwa mwandishi mzuri? Soma sana vitabu. Hii inakuwezesha kuona na kujifunza kutoka kwa waandishi wengine, jinsi wanavyotumia lugha na kujenga mtiririko wa fikra,

7. Vitabu vinakupa maono. Kwanini? Vinatujuza mambo yaliyopita na yanayoendelea kufanyika. Kupitia hayo, tunaweza kujua nini kinaweza kufanyika huko mbeleni. Kuna usemi unaosema "experience leads" yani uzoefu huongoza. Kiongozi mzuri ni yule mwenye uzoefu. Uzoefu humuwezesha mtu 'kunusa' 'detect' mambo yanayoweza kutokea mbeleni.

8. Vitabu vinakukutanisha na watu na kukuza urafiki. Mfano mzuri ni mimi na wewe hapo. Tumeweza kufahamiana kupitia kitabu ulichoandika. Pia wewe na yule mmeweza kufahamiana kipitia vitabu. Pia vitabu vimenikutanisha na wasomaji wa kitabu chako.

9. Hazina kwa vizazi vijavyo. Kusoma kuna faida kuliko kusikiliza. Maana fasihi andishi inadumu kuliko fasihi simulizi. Vitabu ulivyohifadhi kwenye shubaka (shelf) lako sasa hivi, vitasomwa na vitukuu vyako miaka 100 ijayo. Tofauti na hadithi unayosimuliwa sasa, itapotea siku msimuliaji akifa. Teknolojia ya kuhifadhia sauti leo, inaweza isiwepo miaka 100 ijayo.

10. Kiingiacho ubongoni, ndicho kitokacho mdomoni. Hivyo, ukisoma visivyo na maana utazungumza visivyofaa. Lakini, ukisoma vitu vyenye maana, utaongea vitu vya busara. Jenga utamaduni wa kusoma, ubongo wako ni kama 'elastic' kadri unavyojaza vitu ndivyo hutanuka. Afya ya ubongo huletwa na kusoma. Kuna siri nyingi zimejificha kwenye vitabu. "Ukitaka kumficha mtu, weka ujumbe kwenye maandishi".

Wakatabahu
©KichwaKikuu.
Ukweli mtupu!
 
Back
Top Bottom