MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Watu wengi tumekuwa tukipeana ushauri wa biashara zinazolipa hasa kwa wale vijana wadogo wanaoanza pilika baada ya kutoka masomoni. Nimekumbuka biashara kadhaa nzuri ila sio rafiki kwa anayeanza biashara ambaye bado mtaji wake ni mdogo. Haya ni maoni yangu ila sio sheria.
1. Biashara ya kununua mazao wakati wa mavuno na kuyahifadhi kusubiria bei ipande.
Hii sio mbaya kwa watu wenye mtaji mkubwa na pesa nyingi. Tukiachana na risk za mazao kuharibika bali pia kuweka hela chini na kusubiri kwa miezi kadhaa bei ipande inahitaji misuli ya kifedha. Kwa mfanyabiashara anayejitafuta hii sio poa haitamfaa. Mbaya zaidi wakati mwingine bei inaweza isipande.
2. Biashara ya kuagiza vitu China au Dubai na kuviuza Tanzania.
Hii ni nzuri ila unayeanza bora ukazungusha hela yako kwa kununulia vitu kwa wauzaji wa jumla Kkoo na kwingineko hapahapa nchini ili ukuze mtaji. Baadae unaweza anza taratibu kwa kuagiza vitu kadhaa China bila kutumia mtaji wako wote. Tatizo kubwa kwenye hii biashara ni mizigo kuchelewa kufika na wakati mwingine kutumiwa vitu vilivyo chini ya kiwango.
3. Biashara za vitu vinavyoweza kuharibika kwa haraka.
Kwa mfano wale wanaonunua matunda na kwenda kuyauza viwandani hasa pale Mwandege huwa ni risk kubwa. Hata wanaonunua ndizi Moshi na kuziuza Mabibo wana risk sana.
4. Biashara za kampuni inayohitaji vibali vingi mwanzoni.
Kufungua kampuni sio jambo baya kama umejipanga. Ila kama mtaji ni mdogo anza na sole proprietorship badala ya kampuni. Hii itakusaidia kuepuka gharama nyingi za uendeshaji hasa mambo ya kodi. Na hata kama ni kampuni jiulize sana kabla kwasababu kuna kampuni zinahitaji uwe na vibali hadi vya TMDA na TBS.
ONGEZEA ZINGINE KWA FAIDA YA WAFANYABIASHARA WADOGO