Aadilu
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 645
- 463
Namshukuru mola wa viumbe wote baada ya kuhangaika sana mke wangu sasa ni mjamzito. Tangu wiki ya kwanza ya ujauzito wake ambao sasa una wiki takribani tisa amekuwa na tabia ya kuwa na mimi karibu sana. kila wakati anataka tukae pamoja. Hataki nitoke, hataki niwatembelee jamaa na marafiki. Nikitoka kazini tu yeye karibu yangu na macho yetu kwenye TV. Kuna mtu baada ya kumhadithia haya akaniambia mkeo atajifungua mtoto wa kiume. Hivi hii kauli ina ukweli wowote wadau? Mwenye ujuzi jamani anijuze.