Hizi ni kona kali na milima, kwa barabara nchini, taja nyingine

mwanamabadiliko

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2010
Posts
938
Reaction score
1,540
Habari jamvi?, kwa wale wazurulaji nchini

Ukizunguka nchini utakutana na sehemu maarufu , kimandhari na kimuonekano.

Leo naongelea sehemu za barabara nchini ambazo Zina Kona Kali na sehemu ya milima, nataja chache nyingine ongeza

1. Kona za Iyovi - ukitoka tu mikumi kuelekea Iringa utaziona Kona hizi, ni Tamu Sana
2. Kona za kitonga - hizi zinapatikana kutoka Moro kwenda Iringa.

3. Kona za Kolo- hizi zinapatikana kutoka Kondoa kuelekea Babati

4.Kona za Nyang'olo - hizi zinapatikana unapokaribia kufika Iringa kutokea Dodoma

5. Kona za Lukumbulu Songea huko

6. Kona za Msambiazi, Korogwe kuelekea Mombo
7. Kona za Mombo kuelekea Soni - Lushoto
8.Kona za Mbeya kwenda Chunya
9. Kona za Ugara - Babati kwenda Mbulu - hapa kitonga chamtoto Cha ngedele
10. Kona za Hedaru - Vunta, Same

Ni Kona hatari lakini Tamu Sana, na mabasi huwa wanalala na Kona hizi kwa speed ya 120 yaani shaa.

Ongeza Kona Kali nyingine
 
Samahani hiyo namba 4:Nyang'olo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…