Hizi ni kona kali na milima, kwa barabara nchini, taja nyingine

Mkuu funga safari utoke iringa kwenda dodoma au dodoma kwenda iringa via Mtera utakuja kuelezea hiyo kitonga ni cha mtoto
Kitonga imezidi mi nishapita iringa to Dodoma ,songea to dar.njia ya kwenda Dodoma kun kona ila sio nyingi japo ni hatari pia ila kitonga naogopa hadi leo
 
Kona ya Bwiru
 

Barabara ya kutoka Sumbawanga mjini kwenda Bonde la Ziwa Rukwa katika vijiji vya Muze, Mtowisa, n.k. Hebu jaribu kupita barabara hiyo uonee! Huyarudia tena milele! Ndiyo barabara ya hatari kabisa kuliko zote zilizotajwa humu! Moto wa kuotea mbali. Nimesema hivi kwa sababu karibu kona zote za barabara na miteremko iliyotajwa humu naifahamu pamoja na hiyo bsrabara ya Sumbawanga-Muze bonde la Rukwa! Huko si mchezo hata mara moja aisee!
 
Nyang'oro Kona za kawaida sana hizo nilishawahi kushuka na gar ambayo haina uhakika wa brek na nikatoboa
 

Pale juu yaani peak ya hiyo barabara urefu wake ni nusu ya urefu wa mlima Kilimanjaro toka usawa wa bahari. Pana kibao kimeandika mwinuko ni meta 2950 kutoka usawa wa bahari na kuongeza kuwa ule mwinuko ambapo barabara imepita ndiyo mwinuko mrefu zaidi kuliko mwinuko wa barabara yoyote katika Tanzania. Nakubali kabisa hoja yako!
 
Hapo tatizo huwa ni maporomoko ya ardhi (landslides) wakati wa mvua. Ni hatari sana
 

Upo sahihi asilimia 100, hakuna barabara chafu kama hiyo! Na huko bondeni sijui binadamu walifikaje na kuishi huko bondeni huku maana kuna vijiji vingi sana huko! Ila bila kupepesa macho mimi nimewahi kufika bodeni huko mara tano! Hakuna sehemu kama hiyo Tanzania nzima na pengine East and Central Africa nzima!
 
Kuelekea Tarakea/Rongai kuanzia Kibolo je?
 
Kuna kona moja inaitwa KWA SHETANI, njia ya Njombe - Ludewa, hatari sana. Jina linasadifu kona hiyo.

Sijui siku hizi pakoje maana nasikia barabara inakarabatiwa, na sijapita njia hiyo miaka mingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…