Hizi ni kona kali na milima, kwa barabara nchini, taja nyingine

Hakuna barabara yenye kona nyingi za kuudhi kama barabara itokayo Chimala Mbeya kuelekea Matamba na Uwanji Makete.
Kuna kona 54 ukipitia ile barabara ya hifadhi ya msitu wa TFS.
Huko ni balaa ila wengi hawajafika huko ila wakifika watapiga saluti nilipita huko nikiwa na project fulani kutulo shamba la maua pale.
 
Kona za Rombo, Kilimanjaro
 
Daaa Kipindi nasoma Kwiro sekondari hizo Kona za mlima ndororo nilikuwa sizipendi panatisha Sana pale
Hahaha Mlima Nyani....kipindi hauna kipande cha lami..aisee ilikuwa hatari sana.
Kuna jamaa wa Mfundo mwaka juzi alipaa na abiria pale.
 
Hata ile ya Tunduru kwenda Namtumbo ina kona sana. Yaani kona masaa
kona hizi ni hatari, washukuru wamewekewa rami siku hizi, kipindi napiga Pale Tunduru sec ilikuwa mwendo wa vumbi na kona kama zote plus ups n down za kilimasera ilikuwa hapatoshi
 
Ukiacha kitonga na nyang'olo ambazo nazijua kona nyingine ipo njia ya njombe kuelekea makete hiyo nayo ni balaa
 
Kona za mlima kobero

Ukitoka kabanga kuingia border ya burundi
 
Hivi kona za Msambiazi nazo ni kali?
 
Kuna video nimewahi kuangalia youtube njia za huko zilivyo, naona kabisa inaendana na ulichoandika hapa.

Hongera kwa kufika huko mkuu.

 
Kuelekea Mtowisa usipopita Maji Moto kuna mlima mkali sana na korongo panaitwa KABURI WAZI. Nimepita Kitonga,Nyang'olo hadi huko Chunya ila hiyo down ya Kaburi Wazi hakuna mfano sema sio maarufu kwa kuwa sio main.
Ukiteremka chini unadondokea MUZE,,,,,
 
Kuna siku nilipita hapo na KIMOTCO, dereva alikuwa noma sana, speed plus hizo kona, nikabaki kushangaa tu.

Aliomba assist ya overtake kwa dereva wa Lori akapewa na kupaa kileleni kama Bombardier
Duh! Nazani ulihisi haja kubwa inatoka[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ajali hutikea kwa nadra sana, na wanaopata ajali huwa wageni wa njia hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…