Sema TZ hakuna barabara yenye kona mbaya. Tembeeni huko duniani muone maajabu. Last Year i was in Mumbay tukapanga tukatembelee safu ya milima ya Himalaya, mwenyeji wetu Mr Ramesh akatushauri tufanye safari ya kwenda kimji kidogo kiitwacho Mandahli (si mdogo kihivyo ila kwa kule ni mdogo)then tufike sehemu inaitwa Kinnaur and we took a Car instead of a Train which seems to be as cheaper than Car. Kwa Gari mnalipa 1700 Rupee sijui hapa Bongo ni kiasi gani wakati ukitumia Train ni around 900 Rupee. Tuliamua kutumia Gari kwa kuwa mwenyeji alituambia mtaona safu ya hiyo milima kwa uwazi lakn tunapaswa kuwa majasiri wa kiwango kikubwa mno maana ile barabara nadhani inaweza kuwa moja kati ya barabara za kifo zaidi duniani. Safari yetu ilianza mapema saa moja kwa saa za Mumbai (BOMBAY) kuelekea huko ambako ni magharibi ya India na ni mpakani kwa nchi PAKISTANI, CHINA na yenyewe INDIA, huko ndiko hupatikana jimbo maafuru la KASHAMIR ambalo lina mgogoro kati ya INDIA na PAKISTAN na ikumbukwe zamani hizi nchi ilikuwa nchi moja tu. Basi mzigo ukaamshwa na Gari moja matata sana huku sijawahi ona aina hiyo ya gari (MASERATI) aisee asikwambie mtu watu wanateseka kwenye hii dunia acha utani. Hiyo barabara unayopita kwanza nyembamba na mostly haina lami, na ni safari ya siku 2 hivi maana huwazi tembea usiku ile njia wallah. Mnatembea juu ambako chini kuna mto au korongo la urefu wa mita 150 na mkitumbukia huko hakuna atakuja kukutoeni. Muendako mnapaswa kubeba chakula kwa wingi maana hujui kitatukia nn, vyakula vya kihindi michosho kinyama, hawali ng'ombe nk, mi binafsi nilibeba maharage ya kopo, crips, Biskuti nyeupi zinakuwa na chumvi, maziwa na juice. Njiani mnaweza kuta migahawa ile local na sehemu chache vijiji ambako hutoa huduma ya kulala na pancha. Safari yetu ilituchuka siku 3 badala ya 2, mbaya kuna Baridi kali sana kwenye ile safu ya milima na barafu tupu juu huko. Hakuna chance yoyote kwa dereva kufanya makosa yoyote yale, kwanza hakuna vibao vya kuonesha mteremko mkali, au kona ni mwendo wa uzoefu wa dereva tu. Kwa jinsi nilivyokuwa nashikilia gari mungu ndio anajua. Itoshe kusema tembeeni duniani mjionee jinsi madereva walivyo na skills na niseme hapa wazi HAKUNA DEREVA WA TZ ATAENDESHA KWA ILE ROAD.
Next trip mungu akijaalia safari ya Argentina au Peru tutamuomba mwenyeji wetu atutembeze kwenye safu ya milima ya Andes kwa gari ili tujifunze zaidi. Ila pia nasikia CHINA kuna deadly roads sema kwakuwa wako more advanced kwenye technology ndio inapunguza ukali.
TZ hatuna hata barabara inayotisha sema tuna poor technology. Lkn huko India hata namna ya kuweka miundombinu ni mtihani sana.
Kurudi tulirudi kwa Ndege ambayo ni kama rupee 2200 hivi.
Ile barabara hata usisearch kwa Youtube mtajionea ni kama hadithi ila ni kweli kabisa. Wale wahindu wanateseka bhana waacheni waje huku wawe vibarua kwa Mo