Hizi ni kona kali na milima, kwa barabara nchini, taja nyingine

Hizi ni kona kali na milima, kwa barabara nchini, taja nyingine

Mi kona za kitonga aah sijawahi kuzioea kabisa, hasa nikiwa natoka Iringa to Moro (kushuka) huwa nahisi moyo unahama mahali pake huku maini kama yanatoka hivi, aah na madereva sijui ndiyo wamezoea hiyo speed yake sasašŸ¤” huwa nabaki nasali tu na kuminya breki za miguušŸ˜€
Vipi mananii huwa hayagongi chupi
 
Habari jamvi?, kwa wale wazurulaji nchini

Ukizunguka nchini utakutana na sehemu maarufu , kimandhari na kimuonekano.

Leo naongelea sehemu za barabara nchini ambazo Zina Kona Kali na sehemu ya milima, nataja chache nyingine ongeza
1. Kona za Iyovi - ukitoka tu mikumi kuelekea Iringa utaziona Kona hizi, ni Tamu Sana
2. Kona za kitonga - hizi zinapatikana kutoka Moro kwenda iringa.

3. Kona za Kolo- hizi zinapatikana kutoka kondoa kuelekea babati

4.kona za Nyang'olo - hizi zinapatikana unapokaribia kufika iringa kutokea dodoma

5. Kona za Lukumbulu songea huko

6. Kona za msambiazi, korogwe kuelekea mombo
7. Kona za Mombo kuelekea Soni - Lushoto
8.Kona za Mbeya kwenda Chunya
9. Kona za Ugara - Babati kwenda Mbulu - hapa kitonga chamtoto Cha ngedele
10. Kona za Hedaru - Vunta , Same

Ni Kona hatari lakini Tamu Sana, na mabasi huwa wanalala na Kona hizi kwa speed ya 120 yaani shaa.

Ongeza Kona Kali nyingine
Kutoka moshi kuja dar es salaamu kona ziko 2 tuu ya njia panda ya himo naya segera tuu huko kwingine hakuna kona sisi madereva tunanyoosha tuu
 
Habari jamvi?, kwa wale wazurulaji nchini

Ukizunguka nchini utakutana na sehemu maarufu , kimandhari na kimuonekano.

Leo naongelea sehemu za barabara nchini ambazo Zina Kona Kali na sehemu ya milima, nataja chache nyingine ongeza

1. Kona za Iyovi - ukitoka tu mikumi kuelekea Iringa utaziona Kona hizi, ni Tamu Sana
2. Kona za kitonga - hizi zinapatikana kutoka Moro kwenda Iringa.

3. Kona za Kolo- hizi zinapatikana kutoka Kondoa kuelekea Babati

4.Kona za Nyang'olo - hizi zinapatikana unapokaribia kufika Iringa kutokea Dodoma

5. Kona za Lukumbulu Songea huko

6. Kona za Msambiazi, Korogwe kuelekea Mombo
7. Kona za Mombo kuelekea Soni - Lushoto
8.Kona za Mbeya kwenda Chunya
9. Kona za Ugara - Babati kwenda Mbulu - hapa kitonga chamtoto Cha ngedele
10. Kona za Hedaru - Vunta, Same

Ni Kona hatari lakini Tamu Sana, na mabasi huwa wanalala na Kona hizi kwa speed ya 120 yaani shaa.

Ongeza Kona Kali nyingine
Hiyo kulala na 120kph sio kweli.
labda huko Vunta umepataja tu ila hupafahamu kabisa na hujawahi kufika.
 
Kuna mlima Njiwa , Mbeya Vijijini kwenda chunya kupitia ifumbo, kwanza unapita msitu una mashetani na makona Makali na wachawi
 
Kuna kona moja matata kutoka Mbeya kuelekea Malawi imepewa jina Uwanja wa ndege ni balaa,R.I.P nyingi zilipatikana pale hasa kwa wageni enzi hizo hadi kuna kibao cha onyokali,punguza mwendo,tembea taratibu[emoji591][emoji591][emoji591][emoji591]
Hii ilinifirisi. Nimetoka kununua pulling scania. Ikapakia mzigo mara ya kwanza kwenda Malawi. Bahati mbaya bima 3rd party. Ilitumbukia hapo sikuokota kitu.
 
Nyang'olo ni funga kazi ,Kona zaidi ya 80 huku chini unaichunguli ruaha ile ,gari likichumpa tu mnakuwa asusa.
 
Back
Top Bottom