POTOSHI Hizi ni nyumba Rais Ibrahim Traore amejenga kwaajili ya raia wake masikini nchini BurkinaFaso

POTOSHI Hizi ni nyumba Rais Ibrahim Traore amejenga kwaajili ya raia wake masikini nchini BurkinaFaso

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1

Screenshot 2025-09-24 093906.png
 
Tunachokijua
Captain Ibrahim TRAORÉ ni Rais wa kijeshi chini Burkina Faso aliyefanya mapinduzi ya kumtoa Rais wa wa mpito wa wakati huo ambaye alikuwa ni mwanajeshi pia Paul-Henri Sandaogo Damiba September 2022. Aidha Captain Ibrahim anatajwa kuwa miongoni mwa marais wenye umri mdogo zaidi barani Afrika na duniani.

Kumekuwepo na taarifa nyingi potoshi zinazomhusu Rais Traore kutoka nchini BurkinaFaso, moja ya taarifa zinapotosha ni kuhusu kujenga nyumba/makazi kwa ajili ya wananchi nchini humo.

Mfano Mwezi Mei, 2025 kulikuwepo na picha na video zilizosambazwa mtandaoni zikionesha majengo ya ghorofa yaliyodaiwa kuwa ni mradi uliotekelezwa na Rais wa Burkinafaso Kapteni Ibrahim Traoré kwa ajili ya kutoa huduma ya makazi bila malipo kwa raia wa nchi hiyo. Lakini baada ya ufuatiliaji wa kina wa JamiiCheck ilibainika kuwa si kweli na picha na video hizo zilichukuliwa nchini Algeria.

Madai Mengine ya Rais Traore kujenga nyumba kwa ajili ya Raia Masikini.
Kumekuwepo na video inayosambazwa mtandaoni ikionesha nyumba nyingi zilizopangiliwa vizuri zikidaiwa kuwa ni zimejengwa na Rais Rais Ibrahim Traore kwaajili ya raia wake masikini, huku ikisikika sauti inayosema "This is not the United States of America, but is Burkina Faso, Africa"

Je, ni upi uhalisia wa video hiyo?

Kupitia ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia Google Reverse Image Search ulibaini video hiyo ilichapishwa Instagram Februari 28, 2025 katika ukurasa wa Shanghai.dre na China.dre ikiwa na maelezo yanayosema

"Fikiria kuamka katika Kijiji Kipya cha Ma Shan huko Jinan, ambako zaidi ya familia 1,334 zinaishi maisha bora kabisa! Nyumba hizi maridadi za ghorofa mbili si makazi tu ndizo moyo wa jamii inayostawi."

JamiiCheck ilienda mbali zaidi na kutaka kufahamu uhalisia wa eneo hilo kama ndipo zinapopatikana nyumba hizo. Kwa kutumia Google Earth ilibainika kuwa nyumba hizo zinapatikana kijiji cha Mashan eneo la Changqing District nchini China.

Hivyo madai yanayoeleza kuwa nyumba hizo zimejengwa nchini BurkinaFaso, na Captain Ibrahim Traore Rais wa nchi hiyo yanapotosha uhalisia.
​
screenshot-2025-09-24-111616-png.3478181

screenshot-2025-09-24-111453-png.3478182
Watu wanatembea na content tu hawajali ni Ukweli au Potoshi. Mfano Ibrahim Traore ni kweli anafanya kazi ila vitu vingi wanavyosema anafanya siyo kweli
 
Kujengea raia nyumba bure ni kuimarisha uvivu na kusababisha watu wasiwe innovative.
 
Kujengea raia nyumba bure ni kuimarisha uvivu na kusababisha watu wasiwe innovative.
National Housing zilikuwa ni bure au affordable housings ? Nadhani wakusanya Kodi wanapenda sana fikra kama hizi sababu wanawaaminisha kwamba hakuna huduma na hata zile basic needs (chakula na malazi) kuhakikisha kwamba ni affordable sio kazi yao.... : Na kila wakifanya Kazi zao inaonekana kwamba ni Hisani

No wonder wanadiriki kusema uchumi umepanda sababu kuna magari namba E yameongezeka....; Ukiwa na perception ya watu ni nguvu kazi / wazalishaji utagundua kwamba ukihakikisha wana makazi mazuri (sio slums) na wana ujira wa kuweza kuyafanyia maitenance na ukizingatia kuna Kodi za Viwanja na Majengo (hata hio unayoita bure sio bure) na sababu unakusanya Kodi (basi hauwajengei) bali ni katika kuhakikisha unachokusanya kinawasaidia wazalishaji - Building the right infrastructure...
 
Kati ya nchi maskini africa ni burkinafaso , huyu kiongoz anasifiwa na watu wenye mhemko , kiuhalisia burkinafaso bado inahitaji kiongozi
 
National Housing zilikuwa ni bure au affordable housings ? Nadhani wakusanya Kodi wanapenda sana fikra kama hizi sababu wanawaaminisha kwamba hakuna huduma na hata zile basic needs (chakula na malazi) kuhakikisha kwamba ni affordable sio kazi yao.... : Na kila wakifanya Kazi zao inaonekana kwamba ni Hisani

No wonder wanadiriki kusema uchumi umepanda sababu kuna magari namba E yameongezeka....; Ukiwa na perception ya watu ni nguvu kazi / wazalishaji utagundua kwamba ukihakikisha wana makazi mazuri (sio slums) na wana ujira wa kuweza kuyafanyia maitenance na ukizingatia kuna Kodi za Viwanja na Majengo (hata hio unayoita bure sio bure) na sababu unakusanya Kodi (basi hauwajengei) bali ni katika kuhakikisha unachokusanya kinawasaidia wazalishaji - Building the right infrastructure...
Kuwa na affordable housing ni jambo tofauti kabisa na kuwapa nyumba bure kwani wanakuwa hawana uchungu nazo kabisa. Fuatilia hadithi ya Pruitt-Igoe project ilivyofeli spectacularly, utkubali kuwa serikali kutoa nyumba za bure siyo plani nzuri kabisa. Ukitoa affordable housing wakati mkazi anazilipia kodi nafuu, atajisikia yuko responsible.
 
Na dunia ya leo hakuna bure bali unalipia indirectly na ndio maana nimesema kuanzia mwanzo cha maana ni kuhakikisha watu wana ujira; wakiwa na ujira wanaweza kuchukua mortgage kutoka banks (ili kulipia nyumba so long as they are affordable kulingana na kipato chao) Hata wewe leo hicho kiwanja unachosema ni cha kwako bali ni lease ya mpaka miaka 90 (Mmiliki ni Serikali)....; Tatizo kuna huduma ambazo watu tunatakiwa tupate sababu tunatoa Kodi ila ukihoji unaambiwa umezoea bure au ni mjamaa (no wonder hadi Fire na NIDA wanatoa Gawio Serikalini)

Hata hizo affordable housing tunazosema in a closed set they are not affordable (sababu ukisema aje real estate developer atataka apate faida, katika ujenzi (ukizingatia ardhi ndio gharama kubwa; hapa serikali inaweza kutoa bure) na mara nyingi financier ni Benki kwahio kila mtu akishalipwa chake na insurance mwisho wa siku utakuta ni balaa (pesa imetumika nyingi), ambayo inatoka kwenye Kodi yako....; Kwahio cha maana ni kwa Taifa kuona wabangaizaji kama wazalishaji hivyo kuwasaidia katika uzalishaji wao wapate sehemu ya kuishi kwa kuhakikisha kuna system ya mortgage ambayo they can afford.... (instead ya kumpa rent jamaa wajilipie kwa Financier ili mwisho wa siku wamiliki)

Margaret Thatcher UK aliprivatise nyumba za UMMA (council houses) kwa kusema hayo hayo unayosema hapa matokeo yake chini ya Kapeti ni wadau wachache walijimilikisha hizo nyumba kama njugu (kwa bei ya kutupa) na mwisho wa siku kuwachaji hawa downtrodden what they can not afford (mwisho wa siku watu wanaona bora wakawe homeless) ; Na hapa ningeweza kutoa mfano wa Mkapa na Nyumba za Mashirika....

Kwahio narudia it's all about income ya watu kuweza ku-manage makazi yao... maendeleo yote lazima yawe na pillars tatu (Social; Economical na Environmental); Na basic needs hazijawahi kubadilika.... Chakula, Malazi na Mavazi
 
After reviewing theafricareport.com article, my assessment is that the author writes an unbalanced piece, seemingly attempting to disparage the subject while conveniently overlooking crucial historical context.

The article fails to mention how France exploited the country for years, and how Blaise Compaoré was not serving the interests of the people, which ultimately led to the coup
 
Hahaa!

Kwa nini watu wanatumia uongo na uzushi katika kumpamba huyo Traore?

Kama kweli yeye ndiye ‘the real deal’, hizi propaganda za kumpamba ni za kazi gani sasa?

Hana lolote alilofanya lililo la ajabu wala kipekee.

Sifa nyingi anazomwagiwa ni za uongo uongo tu.

Hana tofauti na madikteta uchwara wenzake huko Sahel.

Wote lao ni moja tu.

Wanajilimbikizia madaraka. Wanasogeza mbele muda wa uchaguzi. Na kila aina zingine za figisu ili tu waendelee kuwepo madarakani.
 
Back
Top Bottom