POTOSHI Hizi ni nyumba Rais Ibrahim Traore amejenga kwaajili ya raia wake masikini nchini BurkinaFaso

POTOSHI Hizi ni nyumba Rais Ibrahim Traore amejenga kwaajili ya raia wake masikini nchini BurkinaFaso

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1

Screenshot 2025-09-24 093906.png
 
Tunachokijua
Captain Ibrahim TRAORÉ ni Rais wa kijeshi chini Burkina Faso aliyefanya mapinduzi ya kumtoa Rais wa wa mpito wa wakati huo ambaye alikuwa ni mwanajeshi pia Paul-Henri Sandaogo Damiba September 2022. Aidha Captain Ibrahim anatajwa kuwa miongoni mwa marais wenye umri mdogo zaidi barani Afrika na duniani.

Kumekuwepo na taarifa nyingi potoshi zinazomhusu Rais Traore kutoka nchini BurkinaFaso, moja ya taarifa zinapotosha ni kuhusu kujenga nyumba/makazi kwa ajili ya wananchi nchini humo.

Mfano Mwezi Mei, 2025 kulikuwepo na picha na video zilizosambazwa mtandaoni zikionesha majengo ya ghorofa yaliyodaiwa kuwa ni mradi uliotekelezwa na Rais wa Burkinafaso Kapteni Ibrahim Traoré kwa ajili ya kutoa huduma ya makazi bila malipo kwa raia wa nchi hiyo. Lakini baada ya ufuatiliaji wa kina wa JamiiCheck ilibainika kuwa si kweli na picha na video hizo zilichukuliwa nchini Algeria.

Madai Mengine ya Rais Traore kujenga nyumba kwa ajili ya Raia Masikini.
Kumekuwepo na video inayosambazwa mtandaoni ikionesha nyumba nyingi zilizopangiliwa vizuri zikidaiwa kuwa ni zimejengwa na Rais Rais Ibrahim Traore kwaajili ya raia wake masikini, huku ikisikika sauti inayosema "This is not the United States of America, but is Burkina Faso, Africa"

Je, ni upi uhalisia wa video hiyo?


Kupitia ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia Google Reverse Image Search ulibaini video hiyo ilichapishwa Instagram Februari 28, 2025 katika ukurasa wa Shanghai.dre na China.dre ikiwa na maelezo yanayosema

"Fikiria kuamka katika Kijiji Kipya cha Ma Shan huko Jinan, ambako zaidi ya familia 1,334 zinaishi maisha bora kabisa! Nyumba hizi maridadi za ghorofa mbili si makazi tu ndizo moyo wa jamii inayostawi."

JamiiCheck ilienda mbali zaidi na kutaka kufahamu uhalisia wa eneo hilo kama ndipo zinapopatikana nyumba hizo. Kwa kutumia Google Earth ilibainika kuwa nyumba hizo zinapatikana kijiji cha Mashan eneo la Changqing District nchini China.

Hivyo madai yanayoeleza kuwa nyumba hizo zimejengwa nchini BurkinaFaso, na Captain Ibrahim Traore Rais wa nchi hiyo yanapotosha uhalisia.
​
screenshot-2025-09-24-111616-png.3478181

screenshot-2025-09-24-111453-png.3478182
After reviewing theafricareport.com article, my assessment is that the author writes an unbalanced piece, seemingly attempting to disparage the subject while conveniently overlooking crucial historical context.

The article fails to mention how France exploited the country for years, and how Blaise Compaoré was not serving the interests of the people, which ultimately led to the coup

Traore is refusing to have elections in Burkina Faso, against all democratic norms.

That is an undisputed fact.
 
Back
Top Bottom