Hizi ni sababu tatu kubwa CCM itaongoza milele

Hizi ni sababu tatu kubwa CCM itaongoza milele

Ni kweli lengo kubwa la chama chochote cha siasa duniani ni kushika dola. Ukweli mchungu kwenye hili ni kwamba kwa hapa kwetu Tanzania, bado sikioni hata chama kimoja kati ya vyama vyote 18 ukitoka CCM, ambacho kina msuli wa kuongoza dola.

Zipo sababu kadhaa ambazo kwa maoni yangu, naziona kama sababu ambazo itaifanya CCM itawale milele na milele.

1. Rasilimali
Hili hakuna ambaye hajui kwamba CCM ina mali nyingi sana zinakadiriwa kufikia thamani ya Tsh trilioni 1 za Kitanzania, sidhani kama kuna chama chochote chenye hata theluthi ya utajiri wa CCM.

Uhai wa chama ni rasilimali ilizonazo, dunia ya leo unahitaji fedha kufanya kila kitu. Ili kuwa na chama imara unahitaji mikutano, mitandao ya kijamii, teknolojia na hata washauri wa masuala ya siasa ambapo mambo yote haya yanahitaji fedha nyingi. Vyama vingine hapa nchini dhooful-hal, hawana kitu wanaunga unga hadi fedha za kufanyia mikutano. Hii sio rocket science kushindwa kuelewa kwamba hakuna uhai wa chama kama hakuna fedha.

2. Uzoefu
Hakuna chama kina uzoefu mkubwa wa kuongoza serikali kama Chama cha Mapinduzi. Ukiona taasisi kubwa ya chama cha siasa kama CCM iko madarakani kwa zaidi ya miaka 60, ujue imeshafanya makosa mengi sana, maana yake imejifunza sana kutokana na makosa hayo.

Unajua kwanini kati ya vyama vyote ya ukombozi kusini mwa Jangwa la Sahara vilikubaliana kujenga chuo cha uongozi Tanzania? Hii mada ya siku nyingine.

Nchi zote hizi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, CCM ni maarufu kuliko Tanzania. Kuna wazee ndani ya CCM wanaijua siasa nje ndani, wanazijua fitna zote za siasa, na hata wazee hao wamehusika kuunda vyama vya siasa vya upinzani ambavyo wengi wenu, leo hii mnajivunia kuwa humo, sawa.

Uzoefu wa CCM kwenye siasa za Tanzania kwenye kila kitu ni kigezo ambacho kitaifanya CCM kutawala milele na milele.

3. Connection za Kimataifa
CCM ni chama rafiki wa nchi kama China, Urusi, Cuba na nchi nyingine nyingi tu kubwa la bara Ulaya, Asia na America Kusinia. Hizi nchi zina mchango mkubwa sana kwenye kuifanya CCM kusalia madarakani. Hizi nchi zinakisaidia chama kwa mambo mengi sana, kiteknolojia, kifedha na mambo mengi mengi. Vyama vingine pia tunajua vina marafiki huko nje, bahati ndani njaa na nje njaa.

Hizo ndio sababu kubwa tatu, ingawa ziko nyingi. Kwanini sijaweka sababu ya wanachama? Kwa sababu, wanachama ni sawa na 'Dependent Variable', yaani kuongezeka au kupungua kwake kunategemeana na 'Independent Variable'. Wanachama unaweza usiwe nao leo, ila ukifika wakati wa uchaguzi ukawapata wengi sana. Ukiona chama chako kina watu wengi usipate moyo kwamba unaweza kushika dola, bila fedha, marafiki na uzoefu, unajidanganya.
Acha ujinga... hakuna mamlaka ya kibinaadamu itakayodumu milele.. ila utawala wa Mungu tu.. kama huamini nenda CHATO katizame Kaburi...
 
Kwan wew hujui nn kuhusu madaraka hii ndio maana ya nguvu ,,,, nguvu haetegemei haki pekee hata kma pakihitajika wizi utafanyika ukihitajika uongo utafanyika na hata kama kufa wataua hiyo ndo maana ya nguvu that means ccm wana power ya kuiba kushawishi kuforce kuongoza na kila kitu
Hata wapinzani wanatamani iyo nguvu sema 2 hawana wanatamani ata wao waibe izo kura don't make them very innocent ata mbowe angepata uwanja wa kuiba angeiba tu na hata lisu piah angeiba ili awe raisi sema ndo kazidiwa nguvu
Anyway people have to learn siasa inahitaji nguvu sio kutupigia kelele jukwaani ooh demokrasia😝😝hata izo nchi mnazozifiaga ety zina demo kuna mengi 2 nje ya pazia usitegemee sanduku tu la kura acha ujinga tafuta pesa na nguvu
 
Pamoja na hizo hoja zako,pia naona kama SISIEMU wana media nyingi,na wamezishika kwahiyo propaganda nyingi sana wanaweza kuzipitisha huko,pia Rasilimali watu, kwasasa nchini kwa kuhitaji teuzi mbalimbali wasomi na wamiliki wa baadhi ya makampuni makubwa nchini wanajiassociate na chama tawala ili pamoja na mambo mengine kulinda investment zao na hawa watu wanatoa support kwa Chama hasa Fedha.

NB: Kufa Kwa Sisiemu kutatokana na Sisiemu wenyewe,japo mabadiliko yanaweza kutokea kwasababu wajinga wanapungua nchini
 
Mijini ambapo asilimia kubwa wameelimika Ccm mara zote huwa inaangukia Pua uchaguzi ukiwa huru Na wa haki Ila huko vijijini ndio mtaji wao mkubwa ulipo.
 
Back
Top Bottom