Hizi ni sababu tosha za Hajji Manara kufukuzwa Simba SC

Hizi ni sababu tosha za Hajji Manara kufukuzwa Simba SC

Covid-19

Senior Member
Joined
Mar 2, 2020
Posts
162
Reaction score
364
Kumekua na mgongano mkubwa kwenye club ya Simba juu ya nafasi ya Manara katika club. Mara kadhaa boss wa timu Mo aliihitaji kumfukuza lakini wazee kina Hanspope walimtuliza boss kwamba wampe muda kwani ni mtu muhimu kwenye fan base ya club na hakuna wa kuweza kuziba pengo lake hapa nchini. Msukumo juu ya kufukuzwa kwake umekua mkubwa siku hadi siku na hizi ni baadhi ya sababu zinazoweza kuotesha nyasi kibarua chake muda wowote:

Mgongano wa kimaslahi kati ya Metl na Bakheresa: Ni wazi Mo anachukia sana kwa Hajj kuwa balozi wa Azam akitangaza bidhaa ambazo 99% zinazolishwa pia na Metl. Kama ni mfuatiliaji wa mitandao ya kijamii utakua umeona comments za Mo kwenye Post za matangazo za Manara.

Mgongano wa Kimaslahi kati ya club na Azam tv: Wakati club ikihitaji watu waende uwanjani kujaza uwanja balozi Haji anatangaza namna gani unaweza ku enjoy football ukiwa nyumbani kupitia Azam tv huku ukiwa na ukwaju wa Azam pembeni kwenye sofa.

Ushawishi mkubwa wa Manara kwa mashabiki na wachezaji kuliko mabosi wa Club : Ni wazi kwamba Manara ana ushawishi mkubwa kuliko mtu yoyote pale Simba katika maswala mbalimbali, mfano usajili wa Bernard Morrison 90% umechagizwa na Manara ingawa bodi ilijua tatizo la utovu wa nidhamu wa mghana huyo.

Ushauri: Club imalize swala hili kwa kutumia busara kuliko mihemko.
 
Hakuna taasisi yenye weredi inayoweza kufanya kazi na uyo Albino!! Ujinga, na uswahili umemjaa Sana!! Nashangaa watu wanaosema ana ushawishi!! Sijui ushawishi gani?!! Simbasc ndio imempatia maisha, kabla ya kuja Simbasc alikuwa ana nini?!! Aishukuru Simbasc imempatia maisha ila hana weredi wowote ule!!
 
Huyu Ndiye msemaji no 1 sio TZ bali EA yote.
 
Watanzania bana!! Emu acheni kukuza mambo ya uongo uongo, comments zipi hizo alizotoa Dewji kwa manara? Upo ndani ya club wewe hadi ujue mgongano wa kimaslahi? Alokwambia mpira ni uadui ni nani huyo?

Ukiwa msemaji wa club huezi fanya kazi nyingine zaidi ya hizo? Mwanaume unapofurahia mwenzio kufukuzwa kazi huo ni uchawi pia!! Sometime tujifunze kwa waliotuzidi uwezo ili tufanikiwe, tuache umbea umbea
 
Haji alikuwa bora hadi misimu miwili iliyopita....kwa sasa sifa zimemjaa sana...anafanya vitu hadi vinapitiliza...Mara agombane na waandishi wa habari...Mara atuchanganye kuanza kusifia viongozi wa serikali kwenye mambo ya Mpira...nahisi naye anavizia uteuzi maana ni mwnasiasa huyu na alishawahi kuwa Mwenezi hapa Dsm kabla ya kupiga dili liliomtoa kwenye nafasi hivyo.

Kifupi kwa sasa aachie tu hiyo nafasi na Simba iijaze kwa kuweka wataalam...tuachane na wapiga domo kwani hawaiharibu Simba tu bali mpira.wa tz kwa ujumla wake. Mfano kwa sasa badala ya kujadili soka watu wanajadili kusajili wachezaji wa timu pinzani...

Manara and likes hawatakiwi tena kwenye Soka letu wanaturudisha sana nyuma.
 
Kwa mujibu wa katiba Haji hakupaswa kuwa mwanachama au kiongozi wa simba kwa sababu ya kukosa sifa ya uadilifu kwa wote tunaokumbula ishu yake akiwa katibu mwenezi wa ccm mkoa wa Dar es salaam.

Ila kwa sababu ni mjanja mjanja ndio maana ameachwa lakini kosa lake kubwa wakati anajua yeye ni msemaji wa club na anapaswa kuongea kile kilichoamriwa na club amekuwa akijisahau na kutoa matamko yake binafsi
 
Watanzania bana!! Emu acheni kukuza mambo ya uongo uongo, comments zipi hizo alizotoa Dewji kwa manara? Upo ndani ya club wewe hadi ujue mgongano wa kimaslahi? Alokwambia mpira ni uadui ni nani huyo? Ukiwa msemaji wa club huezi fanya kazi nyingine zaidi ya hizo? Mwanaume unapofurahia mwenzio kufukuzwa kazi huo ni uchawi pia!! Sometime tujifunze kwa waliotuzidi uwezo ili tufanikiwe, tuache umbea umbea
Usipojirekebisha watakutoa mzee. Hiyo barua ya onyo uliyopewa ni ya mwisho.
 
Watanzania bana!! Emu acheni kukuza mambo ya uongo uongo, comments zipi hizo alizotoa Dewji kwa manara? Upo ndani ya club wewe hadi ujue mgongano wa kimaslahi? Alokwambia mpira ni uadui ni nani huyo? Ukiwa msemaji wa club huezi fanya kazi nyingine zaidi ya hizo? Mwanaume unapofurahia mwenzio kufukuzwa kazi huo ni uchawi pia!! Sometime tujifunze kwa waliotuzidi uwezo ili tufanikiwe, tuache umbea umbea
Watu waliofanikiwa hawana mzaha kama Manara, ukiangalia page yake imejaa kejeli, uswahili kujipendekeza kwingi , post zake 20 unaweza kuta zinazo husu team yake ni mbili zingine zote ujinga ujinga tu , usha ona wapi mtu ni rafiki wa kila mtu kama sio u ndumila kuwili eti yeye rafiki wa Alikiba na Diamond, Wema sepetu , Hamisa, Mo, Bahkresa, GSM , kwa hekima gani hio kama sio uswahili?
 
Kitu ambacho watu wengi hawafahamu, akili za Haji manara, Hans Pop na MO zinapishana kidogo sana ndio maana wameweza kufanya kazi pamoja kwa mda mrefu.Kama Simba ingekua na kiongozi anayefanya kazi kwa weredi kwa jinsi Manara anavyo behave asingefikisha wiki angekua amesha fukuzwa.
 
Sasa ww utoporo inawa husu nn?
Au nyie wenye wenye wasemaji wasio kuwa na uswahili timu yenu imefika wapi? utoporo.
 
Utoporo buana sasa nyie wenye wasemaji wenye weeledi wa hali ya juu mmefanya kipi chamaana ndani ya nchi hii?
Watz ni watu wajinga na wenye wivu,na hizi coment zinazo tolewa dhadi ya Manara zina dhibitisha hilo.

Na propaganda dhidi ya manara zimekuwa ziki enezwa na mashabiki wa Utoporo,manyani,mavyura FC, uta dhani litimu lao lilisha fanya jambo lolote la maana zaidi ya kuendekeza uswahili huohuo wanao msemea manara.

Huo uswahili mnao usema ndio umemfanya manara kupata dili za matangazo ambazo zinamuingizia kipato. Utoporo acheni wivu wa kike na Manara bado yupo sana ahendi popote na ataendelea kuwapa sindano mpaka mkome nyie honga honga fc.
 
Back
Top Bottom